Mbunge
wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA) amemvaa Mbunge wa Nzega
Mjini, Mh. Hussein Bashe (CCM) kwa kumpachika sifa ya unafiki baada ya
kutoa kauli ya kwamba hoja zilizojadiliwa bungeni siku ya jana
zinaashiria kuligawa taifa.
Kilichomfanya Nassari kutumia kauli hiyo ya unafiki kwa Hussen Bashe ambapo amejumlisha pia ni sifa ya Wana CCM ni kutokana na Mbunge Bashe kupitia ukurasa wake wa Twitter kusema kwamba amepata hofu juu ya taswira ya viongozi badala ya kujadili mambo kwa msingi ya hoja na kuanza kujadili ukanda.
"Mh.
Bashe aliandika "Bungeni Leo nimeona Un holly discussion ambayo imejaa
dhana ya kuligawa Taifa kwa misingi ya Ukanda na Ukabila.
CCM,Chadema,Cuf na NCCR tuliomo ndani ya Bunge hatuna haki yoyote ya
kuanza kupandikiza mbegu ya kuligawa Taifa".
Ameongeza
"Tanu, CCM toka 1957 mpaka leo ilihimiza Umoja na Utaifa na kukemea
uhalalishaji wowote wa kuligawa Taifa kwa Misingi ya Dini ukanda na
ukabila" Maombi yangu kwa wananchi wenzangu msivumilie mwanasiasa yoyote
yule ikiwa ni pamoja na mimi atakayekuja na hoja yenye lengo la
kuwagawanya" Bashe.
Baada
ya mfululizo wa hoja hizo kwenye ukurasa wa Bashe , Nassari leo amejibu
hoja hizo kwa kumwambia Mbunge huyo kwamba baada ya yeye kushindwa
kumkemea Mwenyekiti wake kwa kutoa kauli zinazotafsiriwa kuwa ni za
kibaguzi ndipo anaibuka na kusema taifa linagawanywa.
"Unafiki
ni moja wapo ya sifa kubwa ya mwanaCCM, HusseinBashe ulishindwa
kumkemea mwenyekiti wako wa chama akitoa kauli za kibaguzi kanda ya ziwa
juu ya bomoa bomoa, leo wanaibuka wabunge kukemea ndio unajitokeza na
kusema tunaligawa taifa?!" Nassari.
Ameongeza
kwamba "Kunyamazia uovu huu kwa kujifanya hatuuoni sio kulisaidia
taifa, ni vyema na ni wakati sahihi kukemea kabla halijamea".
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )