Mwandishi
wa habari wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Rose Athumani
amefariki dunia jana usiku Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Taratibu za mazishi , zinaendelea nyumbani kwa Mjomba wake anayeitwa Pauli Mushi huko Mbezi Mpigi Magohe jijini Dar es Salaam.
Familia hiyo ilisema kuwa Rose alikuwa akisumbuliwa na homa kali iliyosababisha kifo chake kwenye Hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa.
Kwa mujibu wa Mjomba wa Marehemu, shughuli za kuaga mwili zitafanyika Jumapili na Marehemu atasafirishwa kwao Moshi mkoani Kilimanjaro kwa mazishi siku ya Jumatatu.
Marehemu ameacha mtoto mmoja wa Kiume ambaye yuko kidato cha tatu.Marehemu aliwahi kufanya kazi katika Kampuni ya Mwananchi Communications LTDKaimu Mhariri wa Michezo, Zena Chandea alisema kuwa alimfahamu Marehemu Rose tangu mwaka 2009 alipotokea gazeti la The Citizen. Alisema kuwa Rose alikuwa ni rafiki wa kila mtu na alikuwa na tabasamu muda wote.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )