Serikali
imemjia juu waziri wa zamani wa Fedha, Saada Mkuya kwa kutoa
mapendekezo ya kutaka ajira kwa shirika la mawasiliano la simu kwa
upande wa Zanzibar ziwe kwa Wazanzibar.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema
alitegemea hoja ya aina hiyo ingezungumza na watu vijijini huko Pemba au
vijiweni huko darajani Zanzibar na siyo Mkuya.
Profesa
Mbarawa aligeuka mbogo jana Jumanne jioni wakati akijibu hoja
mbalimbali za wabunge waliochangia Muswada wa Shirika la Mawasiliano wa
2017, uliowasilishwa na Profesa Mbarawa.
“Utaratibu
wa ajira TTCL ni Mtanzania yeyote anafanya kazi TTCL. Tunachoangalia
sisi muhimu ni uwezo wa mtu na sifa za mtu. Jambo alilolisema Saada
Mkuya limenisikitisha sana,” alisema.
“Sikutegemea
maneno hayo yangetoka kwa kiongozi kama Saada ambaye alikuwepo
serikalini. Hasa kwa kiongozi ambaye ana uzoefu mkubwa,” alisema Profesa
Mbarawa na kuongeza kuwa;
“Nilitegemea
mawazo au maoni kama yale yazungumzwe na watu wa kijijini kule Pemba.
Nilitegemea mawazo kama yale yazungumzwe na watu wa kijiweni pale
Darajani,”
“Nilitegemea
yeye kama kiongozi na sisi kama Tanzania katika kujenga umoja wetu
tuseme kila Mtanzania afanye kazi mahali popote Tanzania,”
“Mheshimiwa
Naibu Spika hivi tunavyoongea leo, Meneja wa TTCL Zanzibar ni Mzanzibar
anaitwa Mohamed Mohamed. Meneja wa TTCL Pemba ni Mnzanzibar anaitwa
Ngwali Hamis,”
“Naomba
nimpe taarifa mheshimiwa Saada ambaye hazijui kiutendaji. Mtendaji
Mkuu wa TTCL mwaka 2010 hadi 2012 alikuwa Injinia Said Ameir ni
Mzanzibar,”
“Sasa
sikutegemea nasema ni kitu kimeniuma sana. Nilitegemea kama Mtanzania
unatoka Lindi kama kuna fursa TTCL Zanzibar unaenda. Kama Mzanzibar
ameona fursa Kibondo aende.”
“Hii
ndio Tanzania tunayoitaka. Hii ndio Tanzania ambayo Watanzania kule nje
wanaitaka. Nikienda zaidi TTCL tuna TTCL Pesa ina watendaji watano
waandamizi. Watatu ni wanzanzibar”
Jitihada
za Saada kutaka kumpa Profesa Mbarawa taarifa ziligonga mwamba baada ya
Naibu Spika kumweleza kuwa kikanuni waziri akiwa amesimama kwa hatua ya
jana, hakuna taarifa.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )