Serikali
iliwasilisha Muswada wa Sheria ambao unaiua rasmi Kampuni ya Simu
Tanzania (TTCL) na kuanzisha shirika jipya la mawasiliano Tanzania
ambalo litamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100.
Muswada
huo, umewasilishwa bungeni jana Jumanne na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa huku wabunge wakipinga baadhi ya
vifungu vya muswada huo.
Akiwasilisha
muswada huo, Profesa Mbarawa alisema madhumuni yake ni kuanzisha
shirika hilo kwa ajili ya kulinda usalama wa nchi, kukuza uchumi na
kutoa huduma kwa jamii.
Profesa
Mbarawa alisema sheria hiyo mpya itaiwezesha TTCL kutekeleza majukumu
yake kama shirika la umma la mawasiliano likijulikana kama Tanzania Telecommunication Corporation.
Amesema mambo muhimu ya kuzingatiwa katika muswada huo ni kuwa unakwenda kuifuta TTCL na kuanzisha shirika jipya.
Sheria
hiyo ambayo itaumika Tanzania bara na Zanzibar, ilipendekeza muundo
wake na mtendaji mkuu na wajumbe watano ambapo upande wa Tanzania
Zanzibar utakuwa na mjumbe mmoja.
Kwa
mujibu wa sheria hiyo, inaelekeza kwamba ili mtu awe na sifa ya
kuteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu ni lazima awe na uzoefu wa miaka nane
katika ngazi ya juu ya utawala.
Hata
hivyo wabunge waliungana kutaka Zanzibar iwe na wajumbe wawili badala
ya mmoja katika bodi ya wakurugenzi na wakataka pia na uzoefu wa
mtendaji mkuu uwe miaka mitano badala ya saba.
Mbali
na suala la uwakilishi wa Zanzibar, lakini wabunge hao wa CCM na wale
wa upinzani, waliungana pia kutaka waziri asiwe na madaraka makubwa ya
kuingilia uendeshaji wa shirika hilo.
Wabunge
karibu wote waliochangia pamoja kambi rasmi ya upinzani bungeni,
wakapendekeza Zanzibar ipewe nafasi mbili kati ya tano badala ya moja,
ili kuleta sura halisi ya muungano.
Hata
hivyo, Naibu Spika Dk Tulia Ackson alitahadharisha mwelekeo wa mjadala
huo akisema hilo si shirika la kwanza la muungano, hivyo wasije
wakaanzisha utaratibu mpya kwenye mashirika.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )