Mamalaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imesitisha utoaji wa huduma za usafiri kwa
kampuni ya mabasi ya Kilimanjaro Express Limited baada ya kushindwa
kulipa kodi ya Sh500 milioni.
Akizungumza
na gazeti la Mwananchi, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa
TRA, Richard Kayombo amesema wamefikia uamuzi huo baada ya majadiliano
ya muda mrefu na kampuni hiyo kutokuzaa matunda.
Kayombo
amesema biashara ya mmiliki huyo kwa kipindi cha hivi karibuni haikuwa
nzuri kwani mabasi yake 26 yalipungua hadi kufikia 12 lakini si kigezo
cha kutokulipwa kwa kodi ya Serikali.
“Ni
kweli Kilimanjaro Express inadaiwa Sh500 milioni jambo ambalo
lilitufanya sisi kusimamisha shughuli tangu Jumatatu (ya Novemba 13)
hadi hapo atakapolipa kodi anayodaiwa,” amesema Kayombo
Kwa
upande wake, mmiliki wa kampuni hiyo, Roland Sawaya amesema wamezuia
mabasi yake ambayo yalikuwa yameegeshwa katika ghala mjini Moshi mkoani
Kilimanjaro huku akieleza kuwa ni kweli anadaiwa lakini amekuwa akilipa
deni hilo kwa awamu.
Amesema
hivi karubuni alilipa Sh50 milioni na mwezi huu walitaka kulipa Sh35
milioni lakini TRA walikataa na kuwataka kulipa kiasi chote kilichobaki
cha Sh500 milioni huku akieleza kwamba mazungumzo yanayoendelea ana
imani yatafikia mwafaka na kurejea kutoa huduma
Kilimanjaro
ambayo imekuwa ikifanya safari zake kati ya Dar es Salaam, Moshi na
Arusha kwa zaidi ya miaka 20 ni kampuni tanzu ya Kilimanjaro Cargo
Truck.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )