Shirika
la Ndege la Coastal (Coastal Aviation) katika taarifa yake kuhusu ajali
ya ndege iliyotokea jana asubuhi limesema kuwa watu wote 11 waliokuwa
katika ndege hiyo wamefariki dunia.
Coastal
wameeleza kuwa, ndege yao, Cessna Caravan ilipata ajali majira ya saa 5
asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki katika eneo la Empakaai, Ngorongoro
ikiwa na rubani mmoja na abiria 11 wakati ikiwa safarini kuelekea
Serengeti.
Shirika hilo limesema kuwa majina ya waliofariki katika ajali hiyo bado hayajawekwa wazi wakisubiria kuwajulisha ndugu zao.
Mkurugenzi
Mkuu wa Coastal, Julian Edmunds amesema kuwa tukio hilo ni la
kusikitisha sana, na kwamba mara kadhaa amekuwa akisafiri na ndege za
shirikia hilo na hivyo anaimani na marubani pamoja na ndege zao.
Aidha,
ameeleza kuwa kwa niaba ya shirikia hilo na wafanyakazi wake, watafanya
kila litakalowezekana ndani ya uwezo wao kusaidia katika uchunguzi wa
ajali hiyo kwani hakuna kitu cha umuhimu kwao zaidi ya usalama wa
abiria.
Kwa
sasa wameeleza kwamba wanafanya uchunguzi katika eneo la tukio na kuwa,
taarifa zaidi kuhusu chanzo cha ajali hiyo watazitoa mara taarifa
kamili zitakapopatikana.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )