Waziri
mkuu wa zamani, Edward Lowassa amemtumia ‘salamu’ Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa kwamba gharama za kuandaa Katiba Mpya si kubwa ukilinganisha na
mahitaji ya Watanzania.
Akihutubia
mamia ya watu katika viwanja vya Soko Kuu la Kwa Mromboo jijini Arusha
juzi, Lowassa alimsihi Rais John Magufuli kuruhusu mjadala wa Katiba
Mpya kwa kuwa ndiyo kiu ya Watanzania kwa sasa.
“Wananchi
wamesema Rais Magufuli aruhusu mjadala wa Katiba Mpya, lakini waziri
mkuu wake amesema ni gharama sana mimi nasema gharama hizo ukilinganisha
na idadi ya watu wanaohitaji jambo hili ni kubwa sana atukubalie
tujadili Katiba Mpya,” alisema Lowassa huku akishangiliwa.
Baadhi
ya wabunge waliohudhuria mkutano huo ni Godblesss Lema (Arusha Mjini),
Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) na meya wa Jiji la Arusha, Calist
Lazaro.
Lowassa, awali aliwauliza wananchi: “Tunahitaji Katiba Mpya hatuhitaji?” na wananchi walijibu: “Tunahitaji.”
“Mimi pendekezo langu ni kwamba mheshimiwa Rais kwa heshima zote akubali mjadala wa Katiba Mpya,” alisisitiza Lowassa.
Hata
hivyo, Lowassa aliwaambia watu waliohudhuria mkutano huo kuwa jambo
jingine lililomfikisha mbele yao ni kuwashukuru kwa dhati baadhi ya
Watanzania walivyompigia kura mwaka 2015, kwa sababu alizuiwa kuzunguka
nchi nzima.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )