Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema
kuwa aliyekuwa mwanachama wao, Lawrence Masha hakuwa na msaada wowote
ndani ya chama hicho.
Amesema
kuwa kuondoka kwa Masha katika Chama hicho hakijatikisika chochote bali
kinazidi kuimariki na kupokea wanachama wengi wapya, hivyo kuondoka kwa
mtu asiyekuwa na msaada ndani ya chama hicho si tatizo.
“Alikuwa
hatusaidii chochote ndani ya maji, kwani ulishawahi kumsikia amefanya
chochote akiwa chadema? acha amfuate babu yake, acha aondoke zake, sisi
hatujapoteza chochote, hata alipokuwa waziri alifanya nini, acha aende
kwenye biashara zake Uingereza maana tunasikia anawekeza kule,”amesema
Mbowe
\Masha
alitangaza uamuzi wa kuondoka Chadema kupitia taarifa yake
iliyosambazwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ya kuamua
kuachana na Chadema huku akisema chama hicho kinasafari ndefu ya kuweza
kutwaa dola.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )