Rais
Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi
lilipomweka chini ya kizuizi cha nyumbani baada ya leo kuhudhuria
mahafali ya chuo kikuu.
Akiwa
amevalia joho la kisomi lenye rangi za bluu na njano na kofia, Mugabe
mwenye umri wa miaka 93 alikaa kwenye kiti mbele kabisa kwenye ukumbi na
alishangiliwa kwa mbinja na vigelegele alipotangaza kwamba mahafali
yamefunguliwa.
Mkongwe
huyo aliyetawala Zimbabwe tangu ilipopata uhuru mwaka 1980, kwanza
akiwa waziri mkuu (1980 hadi 1987) na baadaye rais (1987 hadi sasa)
aliwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani kwake kuanzia Jumanne ikiwa ni
wiki moja baada ya kumfuta kazi aliyekuwa makamu wake wa rais Emmerson
Mnangagwa.
Hatua
ya kumfukuza kazi Mnangagwa ilichukuliwa na wengi kwamba ulikuwa mpango
wa kumpandisha mkewe, Grace katika nafasi hiyo ya makamu wa rais na
hivyo kumtengenezea mazingira ya kurithi urais wa mumewe.
Zimbabwe
ilibaki imeduwaa baada ya jeshi kuingilia kati katikati ya mzozo mkali
wa kuwania uongozi wa nchi kati ya Grace na Mnangagwa, 75.
Wachambuzi
wa masuala ya siasa wanasema kwamba jeshi linapinga Grace kupanda hadi
kuwa kiongozi wakati Mnangagwa ndiye mwenye uhusiano mzuri na jeshi
hilo.
Mugabe na wakuu wa jeshi wamekutana kwa mazungumzo na hatua yao ya kunyakua madaraka ni ishara kwamba mkongwe huyo anaondoka.
Mnangagwa,
ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuwa kiongozi mpya amerejea nchini baada
ya kutoroka nchi akihofia usalama wake. Jeshi limesema kuwa lilikuwa
katika mazungumzo na Mugabe na litaujulisha umma kuhusu matokeo ya
mazungumzo hayo haraka iwezekanavyo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )