Serikali
imekiri kujitoa kwenye Mpango wa Kimataifa wa uendeshaji wa shughuli za
serikali kwa uwazi (OGP), ambao serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ilijiunga Septemba 21 mwaka 2011.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora,
Mh. George Mkuchika wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini Mh.
Zitto Kabwe lililohoji kwanini serikali imejitoa kwenye Mpango wa
Kimataifa wa uendeshaji serikali kwa uwazi (OGP).
Mh.
Mkuchika amesema baada ya serikali kushiriki kwenye utekelezaji wa
mpango huo kwa muda wa miaka minne imeamua kujitoa, ambapo ameongeza
kuwa sio nchi ya kwanza kujitoa kwenye mpango huo.
“Baada
ya serikali kushiriki utekelezaji wa mpango huo kwa muda wa miaka minne
imeamua kujitoa, na Tanzania sio nchi pekee iliyojitoa, zipo nchi kama
Hungury na Urusi zilijiunga na baadae kujitoa”, amesema Waziri Mkuchika.
Kwa
upande mwingine Mh. Zitto ameshauri kuwa serikali ingeendelea kuwa
mwanachama wa (OGP) ingefaidika kwa sulaa la ndege za Bombadier ambazo
zimekwama nchini Canada kutoka na nchi huyo kuwa ndiyo mwenyekiti wa
sasa wa OGP.
Hata
hivyo Waziri amesisitiza kuwa mahusiano ya Tanzania na Canada ni mazuri
bila hata ya Tanzania kuwa mwananchama wa (OGP) ambapo masuala ya
Bombadier yatashughulikuwa na balozi wa Tanzania nchini humo.
Mpango
wa kuendesha serikali kwa uwazi ulizinduliwa Septemba 20 mwaka 2011 na
rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ikiwa kama taasisi binafsi. Hadi
sasa umoja huo una nchi wanachama 70 ambapo nchi 10 pekee ndio zinatoka
barani Afrika.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )