Wakati
watu wengine wakimuona bundi kama ishara ya uchuro, nuksi na
mikosi, wachawi wao humuona bundi kama kiumbe mwenye hekima na
busara.
Haya si maneno yangu bali ni maneno ya Mganga wa Jadi kutoka nchini Tanzania ajulikane kama MUNGWA KABILI.
Dokta.
MUNGWA KABILI aliyasema maneno hayo hivi karibuni, alipokuwa
akifanya mahojiano ya moja kwa moja kwenye kituo kimoja cha
redio kilichopo jijini Mombasa nchini Kenya.
Maneno
ya Dokta Mungwa yalikuja mara baada ya mwanamama mmoja kutoka
Malindi Kenya kupiga simu akielezea alivyo jawa na hofu kubwa
kwa sababu usiku wa kuamkia siku hiyo, bundi walitua kwenye
mti ulio kuwa kwenye nyumba iliyo jirani yake na kutoa vilio
vya uchuro kwa masaa mawili.
Dokta Mungwa Kabili alikuwa na haya ya kusema :
Pole
sana dada angu kwa masaibu yaliyo kukuta, lakini hata hivyo
usiwe na hofu kwa sababu, si kila mlio wa bundi una maanisha
uchuro. Wakati mwingine bundi hutoa sauti kumaanisha kitu
tofauti kabisa lakini kwa sbabu watu wengi tumeshajiaminisha
kuwa kila bundi aliapo ni uchuro basi tunapotokea na hali hiyo
hujawa na hofu kama ilivyo kutokea wewe.
Kitu
kimoja cha hakika ninacho penda kukujulisha ni kwamba, siku
yoyote utakayo pata kusikia sauti ya bundi, basi jua kuwa
umesikia sauti hiyo kwa sababu bundi wenyewe ndio wametaka
wewe usikie sauti yao. Hii maana yake nini ? Maana yake ni
kwamba, kuna ujumbe ama ishara fulani ambayo bundi wanataka
uipate.
Katika
ndege wote walio umbwa na Mwenyezi Mungu, bundi ndio ndege
pekee mwenye uwezo wa kuruka,kupaa na kutua bila kupiga kelele
wala kutoa sauti yoyote ile. Mungu ameya dizaini mabawa ya bundi
katika namna ya kipekee, namna inayo mfanya bundi aweze kupaa
bila kupiga kelele pamoja na kwamba, kwa kufanya hivyo
huku’nguta mbawa zake.
Bundi anaweza kutua kwenye paa la nyumba yako, akakaa hadi alfajiri na kuondoka pasi na wewe kujua.
Ukiona
umesikia sauti ya bundi, basi tambua ni bundi mwenyewe ndio
amekusudia usikie sauti yake kwa sababu kuna ujumbe maalumu
anataka kukupa.
Wachawi wanamfahamu vizuri sana bundi ndio maana wanampenda sana wala hawashitushwi na mlio wake.
Wachawi wanampenda sana bundi kiasi cha kuiga karibu tabia zote za ndege huyu wa usiku.
Baadhi ya tabia za bundi ambazo wachawi wameziiga ni pamoja na:
1.
Bundi ndio ndege pekee ambae huwa hapigi kelele anapokuwa
anapaa na kutua. Ndege wengine wote huwa wanapiga makelele
pindi wanapokuwa wanapaa kwa sababu ya kupiga mabawa hali
ambayo ni tofauti kwa bundi. Bundi hupaa kimya kimya na hutua
kimya bila mawindo yake kujua. Hii inatokana na jinsi Mungu
alivyo ya dizaini mabawa na manyoya yake ili viweze kumsaidia
kupata ridhiki yake ya kila siku. Wachawi wanapokuwa wanafanya
mipango yao ya kichawi hufanya kimya kimya bila watu wengine
kujua. Na huwa hawataki kabisa kujulikana.
2.
Bundi hutaka sauti yake isikike pale tu anapo amua isikike.
Unaposikia sauti ya bundi jua umeisikia kwa sababu ametaka
uisikie na wala si vinginevyo . Vivyo hivyo wachawi pia hutaka
nguvu zao au mambo yao yajulikane pale tu wanapotaka
vijulikane na si vinginevyo.
3.
Bundi huanza kuruka usiku giza linapo ingia. Vivyo hivyo
wachawi huanza shughuli zao usiku pindi giza linapo ingia.
4.
Sio kwamba bundi hawawezi kuruka mchana . Wakati mwingine bundi
huruka mchana kutafuta mawindo yao na hufanya hivyo pindi
kunapo kuwa na sababu ya msingi kama vile kutafuta chakula
hasahasa katika kipindi ambacho wanakuwa na upungufu wa chakula
au hawakupata mawindo ya kutosha wakati wa usiku.
Vivyo
hivyo wakati mwingine wachawi hulazimika kufanya baadhi ya
shughuli zao nyakati za mchana ingawa uchawi unao fanyika
usiku huwa na nguvu kubwa zaidi kuliko unao fanyika mchana.
5.
Bundi hupenda kufanya shughuli zao usiku wakati mawindo yao
yamelala, vivyo hivyo wachawi hupenda kufanya shughuli zao usiku
wakati wahanga wao wamelala.
6.
Bundi huwa hawajengi vichali vyao wenyewe na badala yake
hutumia vichali vya ndege wawindao mchana kama vile mwewe,
fundi chuma na kunguru. Vivyo hivyo wachawi huwa hawaishi
kwenye nyumba walizo jenga kwa jasho lao wenyewe. Huishi kwenye
nyumba zilizo jengwa na watu wengine, na wao huzimiliki kwa
kutumia nguvu ya uchawi.
Kama
hiyo haitoshi ,wachawi huwa hawahifadhi majini wabaya kwenye
miili yao wenyewe. Hutumia miili ya watu wengine kuhifadhi
majini na mapepo wachafu. Wakati mwingine unaweza kuwa na mapepo
wachafu sio kwa sababu kuna watu wamekutumia ili upate
madhara ila kwa sababu wachawi wanatumia mwili wako kama
kibanda cha kufugia na kutunzia majini yao.
7.
Wakati mwingine bundi hulana wao kwa wao. Bundi wakubwa wenye
pembe kubwa huwala bundi wa saizi ya kati na bundi mbilikimo
vivyo hivyo bundi wa saizi ya kati hula bundi mbilikimo
isipokuwa bundi mbilikimo ndio hawana uwezo wa kuwala bundi
wengine. Vivyo hivyo wachawi hutoa sadaka zap watoto wao ,
waume,wake , wazazi na ndugu zao.
8.
Kwa kawaida bundi huishi hadi miaka kumi . Bundi hutaga mayai
matatu hadi manne na huatamia mayai kwa wiki tatu hadi nne.
Wanapototoa watoto, bundi mbilikimo huwalisha makinda yao kwa
siku 27 wakati bundi wa saizi ya kati na wale bundi wakubwa
wenye mapembe makubwa huyalisha makinda yao kwa muda wa siku 70.
Wanapokuwa wanayalisha makinda yao, huyalisha kwanza makinda
yenye afya na nguvu kisha hufuata makinda dhaifu. Hii maana
yake ni kwamba, kama hakuna chakula cha kutosha, basi makinda
yaliyo dhaifu yatakufa kwa njaa. Vivyo hivyo wachawi katika
kafara zao huwa wanatoa kafara zilizo nona kwanza kisha hufuata
kafara dhaifu.
9.
Bundi hawaoni vitu vya karibu, huona vitu vya mbali tena mbali
sana. Vivyo hivyo Wachawi kwa kutumia rada zao za kichawi
wanaweza wasijue kesho utapatwa na nini lakini wanaweza kujua
utakuja kuwa nani baada ya miaka ishirini ijayo. Ndio maana
huweza kuiba nyota za watu wakingali wachanga.
10.
Ukiachilia mbali nyani na sokwe, bundi ndio kiumbe mwenye sura
inayo fanana sana na sura ya mwanadamu. Hii ni kwa sababu
macho ya bundi yamekaa kama ya mwanadamu. Macho ya bundi
yamekaa kwa mbele na yanaona kitu kimoja kwa wakati mmoja
ilihali ndege wengine macho yao yamekaa pembeni kulia na
kushoto na yanaona vitu viwili kwa wakati mmoja, yani jicho la
kulia linaona kitu kingine na jicho la kushoto linaona kitu
kingine kwa wakati mmoja.
Kwa
sababu hii Mungu amempa bundi shingo yenye uwezo wa kuzunguka
mbele nyuma . Unapopita kwenye mti ambao bundi ametua
atakutazama, ukimpita katika usawa wake wa machoi atageuza macho
yake na kukutazama hadi mwisho wako. Wachawi pia hufanya vivyo
hivyo. Unapowapita katika vijiwe vyao,watakutazama hadi utakapo
malizikia.
11.
Bundi hufumba macho kama mwanadamu yaani kutoka juu kwenda
chini tofauti na ndege wengine wote ambao wao hufumba macho
kutoka chini kwenda juu.
Na
Sio kweli kwamba bundi hawaoni mchana, bundi wanaona mchana
vizuri sana tu, ila kwa sababu macho yao ni makubwa na makali
sana yenye uwezo wa kuona mara saba zaidi ya mwanadamu, usiku
kwao huwa kama mchana kwetu ndio maana hupendelea zaidi kuwinda
usiku. Wachawi hutoka usiku kuwanga sio kwa sababu hawaoni
mchana. Hufanya hivyo kwa kumuiga bundi.
12.Bundi
anapokutana na hatari hutuna na kuwa mkubwa mara mbili ya
ukubwa wake wa asili. Mchawi anapokutana na changamoto yoyote
katika shughuli zake za kichawi huenda kutafuta msaada kwa
wachawi wenye uwezo mkubwa mara mbili zaidi yake.
13.Bundi
huwa na mkia mfupi sana kiasi kama huwajui bundi ukimuona
kwa ukaribu zaidi kwa mara ya kwanza unaweza kudhani mkia
umekatwa. Wachawi huwa na mawazo mafupi sana. Mfano Wachawi
hutumia mkia wa bundi kufanya shughuli mbalimbali za kichawi
kama vile kufupisha maisha ya maadui zao, au kufunga maumbile ya
kiume yawe mafupi, kufunga mahusiano yawe mafupi nakadhalika.
14.
Pamoja na kwamba bundi wana tofautiana ukubwa wa maumbile,
yaani wakubwa, saizi ya kati na wadogo ama bundi mbilikimo,
lakini bundi wote wana sifa zinazo fanana, mfano bundi wote
huwa na vichwa vikubwa kuliko maumbile yao, wote wana manyoya
laini, wote huwa na mikia mifupi sana, wote huwa na rangi ima
ya kahawia au ya kijivu , huwa na milio inayo fanana, huruka
na kupaa kimya kimya, huwa na manyoya kwenye miguu. Vivyo hivyo
wachawi pamoja na kwamba, wanaweza kuwa na nguvu na madaraja
tofauti katika uchawi,lakini wote huwa na tabia zinazo fanana
kama vile chuki, husda, unafiki , roho ya mbaya,mawazo mafupi
nakadhalika.
15.
Pamoja na kwamba bundi wote huanza kutafuta mawindo yao pindi
giza linapoingia, lakini hutoka kwa nyakati tofauti tofauti.
Mara nyingi huanza kutoka bundi mbilikimo. Hawa bundi mbilikimo
hasa wale wanaoishi porini hutoka kuanzia saa 4 usiku, bundi wa
saizi ya kati hutoka kuanzia saa sita usiku na bundi wenye
pembe kubwa hutoka kuanzia saa nane za usiku . Wachawi nao
wanapo kuwa wanaenda kuwanga na kufanya shughuli zao za
kichawi nyakati za usiku hupishana nyakati. Ingawa vikundi vingi
vya kichawi huanza kutoka kuanzia saa sita usiku, lakini
hupishana. Vingine hutoka saa saba , vingine saa nane. Tofauti ni
kwamba karibu wachawi wote hurudi majumbani mwao nyakati sawa.
Hata
hivyo, bundi hutoka kwa nyakati tofauti kwa sababu maalumu. .
Bundi karibu wote wakubwa kwa wadogo hushea vichali na huishi
katika eneo moja. Hutoka kuwinda nyakati tofauti tofauti kwa
ajili ya kupunguza ushindani wakati wa mawindo..
16.
Pamoja na kwamba macho ya bundi yana nguvu sana lakini
wanapokuwa katika mawindo hutumia zaidi masikio yao kuliko macho
yao. Masikio ya bundi yana nguvu sana na huweza kusikia hata
sauti ya kitu kilicho umbali mrefu sana. Hata hivyo bundi
wanapokuwa wanaenda kuwinda wakati wa mchana hutumia macho
zaidi kuliko masikio. Vivyo wachawi, huamini zaidi vitu wanavyo
visikia kuliko wananvyo viona. Yaani mchawi kila anacho ambiwa
kuliko kile alicho kiona. Kwa mfano wewe A una ujauzito hata
wa miezi sita. Lakini kwenye kilinge cha wachawi alipoenda
kukuroga ,ukapewa jina kuwa wewe ni MGUMBA. Basi mchawi
ataendelea kukuita na kukuchukulia na kuamini kuwa wewe ni
mgumba. Ataendelea kuamini hivyo hata kama utazaa watotyo kumi.
17.
Bundi wanapokuwa wanapaa huutawala upepo na anga. Wana mamlaka
juu ya anga , na upepo. Vivyo wachawi wanapo kuwa wanapaa huamini
kuwa wana mamlaka juu ya anga na upepo kama alivyo bundi.
18.
Bundi huzungusha kichwa kupima umbali wa anapotaka kuruka vile
vile wachawi hupima nguvu ya kiroho ya mtu kabla ya kumtupia
uchawi.
19.
Ukiachilia mbali bundi wanao kula wadudu, bundi wengi huwa
hawana tabia ya kuhama hama. Wanaweza kukaa katika eneo moja
kwa zaidi ya mwaka mmoja. Wachawi pia huwa hawami hami. Huweza
kukaa katika mtaa mmoja kwa zaidi ya miaka arobaini. Na
wanapokuwa wanatengeneza uchawi wa kuwatuliza wanaume kimapenzi
hutumia vichali vya bundi walio kaa kwenye kichali hicho kwa
muda wa mwaka mmoja na zaidi.
20.
Wakati mwingine bundi hupenda kuwinda wadudu wanao tembea
usiku ili kuwa na uhakika wa kupata kitoweo. Wadudu hao ni
popo. Vivyo hivyo wachawi wakati mwingine hufanya ulozi nyakati
za usiku katika maeneo au mazingira ambayo walengwa wao
wanakuwa macho ili kuwa na uhakika wa kupata mawindo yao.
Mfano ni kwenye klabu za usiku zinazo kesha, kwenye misiba au
sherehe zinazo kesha nakadhalika
21.
Tunafahamu kuhusu uwepo wa bundi pindi wanapo toa milio na
sio pindi wanapokuwa kimya. Vivyo tunafahamu kuhusu uwepo wa
wachawi katika mazingira tunayo ishi pindi wanapo tupa uchawi
wao na sio wanapokuwa hawajatupa uchawi.
22.
Bundi wakubwa hutoa sauti kubwa kuliko bundi wadogo. Vivyo
hivyo, wachawi wadogo hujulikana zaidi kuliko wachawi wakubwa.
KWANINI WACHAWI WANAMPENDA SANA BUNDI
Wachawi
wanampenda sana bundi kwa sababu wana amini bundi ni kiumbe
mwenye faida nyingi sana kwao. Baadhi ya mambo ambayo
wachawi huya amini kama faida zinazo letwa na bundi ni kama
ifuatavyo :
1.Bundi
huwasaidia wachawi kuchunga misukule yao ; Katika ulimwengu wa
wachawi mtu aliye chukuliwa msukule mara baada ya kukatwa
ulimwi hatua inayo fuatwa huwa ni kulishwa vumbi la mifupa
iliyo temwa na bundi. Dawa hiyo huufanya msukule huo usahau
kila kitu ulichokuwa unakijua kabla ya kuchukuliwa msukule.
Kwa
wasio fahamu, bundi huwa wanakula wadudu na wanyama mbalimbali
kama vile nyoka, nge,panya, pimbi, panyabuku, ndezi, popo na hata
samaki. Bundi huwa wanakula vitu vizima vizima na kutema
mifupa yao. Sasa hii mifupa inayo temwa na bundi ndio wanayo
itumia wachawi kuwalisha misukule wao kwa minajili ya
kuwafanya wasahau kila kitu walichokuwa wanakijua kabla hawaja
chukuliwa msukule pamoja na kuwapa uwezo wa kuona mambo yasiyo
onekana na kutokuonekana na watu wa kawaida.
2. Bundi huwasaidia wachawi kulinda mashamba yao dhidi ya wadudu waharibifu wa mazao
Moja
kati ya shughuli kuu za wachawi ni kilimo kwa kuwatumia
misukule. Kwenye mashamba huwa kunakuwaga na panya waharibifu wa
mazao . Na kama nilivyo sema hapo mwanzo kuwa, moja kati ya
yakula vinavyopendwa sana na bundi ni panya. Kwa wastani bundi
mmoja anaweza kula hadi panya elfu moja kwa mwaka. Mchawi
akiwakaribisha bundi ishirini kuwa wanatembelea kila siku
shambani kwake maana yake ni kwamba ndani ya mwaka mmoja
watakuwa wamemsaidia kula panya elfu ishirini ambao wanaweza
kuharibu hadi tani 31 za mazao.
Hivyo
basi kwa wachawi hapo bundi huwa msaada wao mkubwa wa
kiuchumi. Huwasaidia kutunza na kulinda mashamba yao dhidi ya
wadudu waharibifu. Huwasaidia kuokoa gharama za kununua dawa za
kuua wadudu waharibifu ambazo zingeweza kuwagharimu mamilioni ya
shilingi.
3.Bundi huwasaidia wachawi kuondokana na madhara ya wadudu hatari kama nyoka na nge
Bundi
ni walaji wazuri sana wa wadudu hatarishi kwa binadamu kama
vile nyoka na nge. Hivyo kwa mchawi kuwakaribisha bundi shambani
kwake au nyumbani kwake anakuwa amejihakikishia kuwa hawezi
kupatwa na madhara ya kuumwa na nyoka au nge kwa sababu bundi
wanapoweka makazi yao katika eneo lolote lile, nyoka hawawezi
kukaa mahali wapo.
4. Bundi huwasaidia wachawi katika shughuli mbalimbali za kichawi.
Kwa kutumia maarifa ya kichawi, wachawi humtumia bundi katika shughuli mbalimbali zap kichawi kama vile :
i.
Kwenda kuzimu : Bundi ni mesenja wa kuzimu na dunia. Huchukua
habari za kuzimu na kuzileta duniani na habari za duniani
huzipeleka kuzimu . Bundi ni daraja linalo unganisha kuzimu na
duniani. Ni daraja linalo unganisha ulimwengu usio onekana na ule
unao onekana. Kwa wale wasio fahamu, umbali kutoka duniani na
kuzimu ni kilomita sifuri. Moja kati ya mawakala wa malango
makuu yanayo unganisha dunia na kuzimu ni huyu ndege aitwae
bundi.Ukaribu na urafiki wa wachawi kwa ndege huyu
unawanufaisha wachawi na kuzimu
ii.
Kuiba na kuharibu nyota za watu hususani watoto wachanga :
Wanapokuwa katika mchakato wa kuiba nyota za watu hususani
watoto wachanga, wachawi humtumia bundi kufanikisha mchakato.
KWANINI
WANAMTUMIA BUNDI : Bundi ana sifa moja kubwa sana. Hana uwezo
wa kuona vitu vya karibu lakini ana uwezo wa kuona vitu vya
mbali sana. Hiyo ni sifa yake katika ulimwengu wa nyamja ambayo
ina sadifu sifa na uwezo wake katika ulimwengu wa roho. Katika
ulimwengu wa roho bundi ana uwezo wa kuona na kujua mambo
yatakayo mtokea mtu miaka 30 hadi sitini ijayo.
Bundi anaweza kuona kifo cha mtu miaka kumi mbele, siku moja mbele, siku mbili mbele, wiki nakadhalika.
Hii
ndio sababu inayo mfanya bundi kutoa taarifa kwa mhusika,
ndugu, jamaa na marafiki zake siku kadhaa kabla ya kifo cha mtu
huyo.
Bundi
hufanya hivyo kwa kutoa mlio maalumu. Wachawi kwa sababu
wanafundishwa namna ya kuwasiliana na bundi, bundi anapotoa mlio
wa kuashirikia kutokea kwa msiba, mchawi na yeye hupiga mluzi
ima kwa mdogo ima kwa filimbi ya kichawi kumjibu bundi, na
bundi asipo jibu mlio huo, basi mchawi anakuwa amejua kuwa
siku zake zap kuishi hapa duniani zimefika ukingoni.
Mtoto
anapozaliwa, wachawi kwa kutumia uchawi na nguvu za kiroho zap
bundi hupeleka jina la mtoto huyo ili kujua atakuwa nani
baadae, na endapo itajulikana kwamba mtoto huyo atakuwa mtu
mkubwa mwenye mafanikio, basi nyota yake itaibwa mara moja.
Nyota hii inapochukuliwa ima, huuzwa kwa mtu, hutumikishwa msukule, ama kuzikwa.
Nyota
ya mtoto mchanga inapo chukuliwa, hubadilishwa na nyota chafu
na matokeo yake mtoto huyu anaanza kuishi maisha ambayo si
yake.
Vile vile kwa kumtumia bundi, wachawi huweza kurudisha nyuma jambo baya ambalo lingemtokea mtu miaka ya mbeleni.
Kwa
mfano ramani yako ya maisha inaonyesha kuwa utafariki kwa
maradhi ya kisukari ukiwa na miaka 75. Wachawi kwa kumtumia
bundi wanaweza kuyarejesha nyuma maradhi hayo na kukufanya
uyapate ukiwa na miaka thelathini.
Mambo mengine ya kichawi ambayo wachawi huwatumia bundi kuyafanya ni pamoja na :
1. Mavi ya bundi hutumika kwenye ungo wa kusafiria kichawi
2.
Mavi ya bundi huchanganywa na mavi ya chatu, sokwe, nyani, maji
ya maiti, mavi ya mtu aliye jisaidia akiwa porini pamoja na
madawa mengine, katika kumtia mtu mikosi.
3. Matambiko ya biashara na madini migodini
4.
Hutumika kufungua milango ya kuzimu wakati wa kuvuka kutoka
duniani kwenda kuzima kwa njia ya kupitia baharini.
5.
Kuwa na uwezo wa kuona wachawi, kuona mambo yaliyo jificha,
mambo yatakayo tokea mbeleni, mambo ya
siri.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )