TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
IJUMAA
TAREHE 10 NOVEMBA, 2017 Mbele ya MHESHIMIWA JAJI LUGANO MWANDAMBO ,
MAHAKAMA KUU YA DAR ES SALAAM imetoa maamuzi (Ruling) juu ya Maombi ya
Zuio (Temporary Injunction) dhidi ya Lipumba na wenzake 14 katika Shauri
dogo la madai [MISCELLENEOUS CIVIL CASE NO. 447/2017] USHINDI ULIOUPATA
CUF NA WABUNGE WAKE 8 NA MADIWANI 2 kutoka Mahakama Kuu ni kama
ifuatavyo;
1.
Mahakama Kuu IMETENGUA KUFUKUZWA KWAO UANACHAMA NA IMESITISHA
UTEKELEZWAJI WA KUFUTWA KWAO UANACHAMA mpaka pale shauri la msingi
litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.
2.
Mahakama imemzuia Lipumba, Magdalena Sakaya na Bodi ya Wadhamini ya CUF
[Bodi FEKI iliyosajiliwa na RITA] na au Wakala wao yeyote KUJADILI juu
ya uanchama wa Wabunge 8 na Madiwani 2 mpaka pale shauri la msingi
litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.
3.
Mahakama Kuu imekubaliana na HOJA ZA Wabunge 8 wa CUF [WAPELEKA MAOMBI
-APPLICANTS] KWAMBA; imeona kuwa Zipo HOJA ZA MSINGI ZA MADAI YAO
ZINAZOPASWA KUANGALIWA JUU YA UHALALI WA MASUALA YOTE HAYO
YALIYOWASILISHWA MBELE YAKE.
4. Mahakama Kuu imeyatupilia mbali mapingamizi mengine yote yaliwekwa na Lipumba na Wenzake katika shauri hili.
Haya
ndio maamuzi ya msingi yaliyotolewa na MAHAKAMA KUU. Maamuzi haya
tafsiri yake ni kwamba kile alichokifanya SPIKA WA BUNGE Job Ndugai ni
BATILI, NA WABUNGE 8 NA DIWANI 1 WA MANISPAA YA TEMEKE WALIOAPISHWA NI
BATILI KWA KUWA WAHUSIKA WOTE BADO NI WANACHAMA HALALI WA THE CIVIC
UNITED FRONT[CUF-CHAMA CHA WANANCHI]. NI KWA MSINGI NI HUO Hatua na
taratibu za kisheria zitachukuliwa kuhakikisha kuwa HAKI INAREJESHWA KWA
WENYE KUSTAHIKI NAYO NA WABUNGE WA LIPUMBA WATATOKA BUNGENI.
Aidha,
Mahakama Kuu imekubaliana na hoja za Mwanasheria wa Manispaa wa Ubungo
na Temeke juu ya utaratibu uliotumika Manispaa zao kufikishwa Mahakamani
hapo kuwa haukufuata taratibu za kisheria na kwamba Mahakama haina
Mamlaka kwa mujibu wa Sheria kuchunguza Maamuzi yaliyofanywa na Tume ya
Taifa ya Uchaguzi [NEC] kwa Mujibu wa Katiba na Sheria.
MAHAKAMA
KUU IMEFUNGUA MLANGO WA KUSHUGHULIKIA Shauri la msingi (CIVIL CASE NO.
143/2017) Lililopangwa kusikilizwa/kutajwa Tarehe 13/2/2017 kati ya
Wabunge wetu 8 ambao ndio WADAI [APPLICANTS]
1. MIZA BAKARI HAJI
2. SAVERINA SILVANUS MWIJAGE [MBUNGE]
3. SALMA MOHAMED MWASA [MBUNGE]
4. RAISA ABDALLAH MUSSA [MBUNGE]
5. RIZIKI SHAHRI NG'WARI [MBUNGE]
6. HADIJA SALUM ALLY AL QASSIM [MBUNGE]
7. HALIMA ALI MOHAMED [MBUNGE]
8. SAUMU HERI SAKALA [MBUNGE]
9. ELIZABETH ALATANGA MAGWAJA- DIWANI VITI MAALUMU MANISPAA YA TEMEKE.
10. LAYLA HUSSEIN MADIBI- DIWANI VITI MAALUM-MANISPAA YA UBUNGO.
DHIDI YA WADAIWA [RESPONDENTS]
1) BODI YA WADHAMINI -CUF,
2) MWENYEKITI WA CHAMA TAIFA,
3) KAIMU KATIBU MKUU-CUF,
4) MKURUGENZI TUME-NEC,
5) KATIBU WA BUNGE,
6) MKURUGENZI MANISPAA- TEMEKE
7) MKURUGENZI MANISPAA -UBUNGO
8) RUKIA AHMED KASSIM,
9) SHAMALA AZIZ MTAMBA,
10) KIZA HUSSEIN MAYEYE,
11) ZAINAB MNDOLWA AMIR,
12) HINDU HAMIS MWENDA,
13) SONIA JUMAA MAGOGO,
14) ALFREDINA APOLINARY KAHIGI,
15) NURU AWADH BAFADHILI
HOJA ZA WABUNGE WETU :
1. Wabunge na Madiwani Wetu walikuwa wanadai HAKI YA UANACHAMA WAO ambayo tayari leo imerejeshwa kwao.
2.
Wanahoji jinsi mchakato uliotumika kufikia maamuzi ya kuwavua uanachama
kwa mujibu wa Katiba ya CUF na huku kukiwa na mashauri ya msingi
yanayoendelea mahakamani yanayohoji uhalali wa Uongozi juu ya ‘Mgogoro
uliopandikizwa na Vyombo vya dola kwa kumtumia Msajili wa Vyama vya
siasa nchinji unaoendelea.
3.
Wanahoji juu ya uhalali wa vyombo vilivyochukua hatua hizo za nidhamu
dhidi yao kama zimefuata taratibu ikiwa ni pamoja na kuwapatia taarifa
rasmi za tuhuma zao kwa maandishi, siku na tarehe ya kikao hicho, kupata
nafasi ya kujitetea, huku ikizingatia kuwa si wote wanaoishi Dar es
Salaam, kulikofanyika kikao cha maamuzi.
4. Uharaka wa Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua hatua bila kujiridhisha vyakutosha.
5. Kutokupewa nafasi ya kusikilizwa na kujitetea kwa mujibu wa Katiba ya CUF na vikao kuendeshwa kwa speed ya mwendokasi-‘DART'
6.
Maamuzi hayakuzingatia haki za kikatiba za mwanachama ikiwemo haki ya
kukata Rufaa ndani ya siku 14 Ibara ya 108(5) ya katiba ya CUF, Mkutano
Mkuu ndio wenye mamlaka na maamuzi ya mwisho juu ya masuala yote ndani
ya Chama.
7.
Je Vyombo vilivyowachukulia hatua za kinidhamu vina uhalali wa Kikatiba
ndani ya CUF? Hayana mengine mengi ndiyo yanayohojiwa Mahakamani katika
shauri hili la msingi.
Tunapenda
kuchukua fursa hii kuwapongeza Mawakili wetu Wasomi Peter Kibatara na
Omary Msemo kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kulisimamia suala hili kwa
weledi mkubwa. Tunawapongeza Viongozi wa CUF wa ngazi mbalimbali za
Chama, Wanachama, Madiwani na Wabunge wote waliokuwa pamoja na CHAMA NA
AMBAO HAWAKUKUBALI KUYUMBA WALA KUYUMBISHWA kwa kufanikisha na kusimamia
mapambano haya ya kisheria. Tunaamini na hivyo ndivyo itakavyokuwa
kwamba HAKI NA USHINDI VIPO KARIBU KUPATIKANA.
JAJI NDYASOBERA ATOA AMRI YA KUITWA WAJUMBE BODI YA RITA:
Katika
hatua nyingine ya mapambano ya kisheria Jumatatu Tarehe 13/11/2017
Mbele ya Mheshimiwa Jaji Ndyansobera, Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini FEKI'
ya Lipumba wameitwa Mahakama Kuu kwenda kujieleza MMOJA MMOJA juu ya
uhalali wao.
CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.
HAKI SAWA KWA WOTE
Imetolewa leo Tarehe 10/11/2017
Na. Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )