Serikali
inatarajia kuanzisha mfumo mpya wa elimu hapa nchini ambao elimu ya
msingi itakuwa inatolewa kwa miaka 6, tofauti na ilivyo sasa ambapo
hutolewa kwa miaka 7.
Akijibu
swali linalohusu watoto wa kike kuolewa wakiwa na cheti cha kuhitimu
elimu ya sekondari, Naibu Waziri wa TAMISEMI Mheshimiwa Joseph Kakunda
ametolea ufafanuzi suala hilo na kusema kwamba mfumo huo mpya utatoa
fursa kwa wanafunzi wa elimu ya msingi kusoma miaka 6, huku chekechea
ukiwa ni mwaka mmoja na sekondari ni maka minne, ambayo itakuwa ni
lazima.
“Napenda
kutoa majibu sahihi waliopata mkanganyiko, nilisema sera mpya ya elimu
huko tunakoelekea inabadilisha mfumo wa sasa wa elimu ambao utahitaji
mtoto aanze chekechea mwaka mmoja, elimu ya msingi miaka 6, sekondari
miaka minne na itakuwa ni lazima”, amesema Mheshimiwa Kakunda.
Mheshimiwa
Kakunda ameendelea kwa kueleza kwamba kutokana na mfumo huo mpya ambao
utaruhusu mwanafunzi kusoma kwa muda mfupi, na baada ya kuhitimu ndio
utakuwa kithibitisho pekee kwamba binti amemaliza elimu ya sekondari na
ndipo ataruhusiwa kuolewa.
Hivi
karibuni Waziri kakunda alitoa taarifa ikisema kwamba ili mtoto wa kike
aweze kuolewa atahitaji kuwa na cheti cha kuhitimu sekondari, suala
ambalo liliibua mjadala kwa wananchi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )