Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jafo amemsimamisha kazi
Mkurugenzi wa Wilaya ya Nkasi, Julius Kawondo kwa tuhuma za rushwa na
matumizi mabaya yaliyoisababishia Serikali hasara ya Sh 7 bilioni
Jafo
amewaambia waandishi wa habari jana Ijumaa kuwa Kawondo ameshindwa
kusimamia kile alichopaswa kukifanya kwa wakati katika eneo lake la
utumishi.
"Natumia
Sheria ya Serikali za Mitaa Sura ya 4 kifungu cha kwanza hadi tano
pamoja na Sura ya 287 ya sheria hiyo ambavyo vinanipa mamlaka hayo,"
alisema Jafo.
Alisema
fedha hizo zilikuwa za mradi wa maji wa Kijiji cha Kamwanda ambako
mkurugenzi alishirikiana na mmoja wa maofisa kutoka wizara ya maji.
Jafo
alimuomba Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe kumchunguza
mmoja wa watumishi katika wizara yake ambaye alishirikiana na mkurugenzi
huyo kuhujumu mradi wa maji katika Kijiji cha Kamwanda wilayani humo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )