Mbunge
wa Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe amefunguka kuwa ndani ya chama
chake (ACT) kuna watu wengi wakiwemo wanachama wa kutosha akimaanisha
hajabaki mwenyewe.
Zitto
amefunguka hayo akimjibu mfuasi wake wa kwenye mtandao wa kijamii
ambaye alitoa maoni yake kwa kumuuliza Mh. Kabwe haoni kama amebaki peke
yake, ikiwa ni muda mfupi baada ya aliyekuwa Mgombea urais wa chama
chake Anna Mghwira kujiunga na CCM huko Dodoma.
Akimjibu
mfuasi huyo Zitto amesema "Chama chetu ACT Wazalendo kina madiwani 42,
kina wenyeviti wa mitaa, vitongoji na wajumbe wa Serikali za
Vijiji/Mitaa 507, Viongozi kila mkoa na jimbo, wajumbe wa Kamati Kuu,
Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu. Ni dhahiri tuna watu wengi na wanachama
wengi wa kutosha"
Hivi
karibuni CCM ilijivunia wanachama wapya ambao waliwahi kuwa na nafasi
ya uongozi ACT Wazalendo ambapo baadhi yao ni Prof Kitila Mkumbo, Samson
Mwigamba, Alberto Msando na jana Anna Mghwira.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )