Wabunge
Susan Kiwanga na Peter Lijualikali waliofikishwa katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Morogoro pamoja na washtakiwa wengine 36 wamerejeshwa
rumande.
Mahakama
iliyokuwa itoe uamuzi wa dhamana leo Jumanne Desemba 5,2017 imekwama
kufanya hivyo kutokana na kuibuka hoja za kisheria.
Upande wa mashtaka na ule wa utetezi unavutana kuhusu hati ya kiapo ya kupinga dhamana iliyowasilishwa mahakamani hapo.
Kutokana
na mvutano wa kisheria, hakimu Ivan Msack ameahirisha kesi hiyo hadi
kesho Jumatano Desemba 6,2017 ili kutoa fursa kwa pande zote mbili
kujibu hoja kuhusu hati hiyo.
Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka nane likiwamo la kuchoma moto ofisi ya Kata ya Sofi iliyopo wilayani Malinyi.
Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka nane likiwamo la kuchoma moto ofisi ya Kata ya Sofi iliyopo wilayani Malinyi.
Washtakiwa wanatetewa na mawakili Peter Kibatala, Ignas Punge, Fredrick Kiwelo na Bartholomew Tarimo.
Upande wa mashtaka unawakilishwa na mawakili wa Serikali, Edga Bantulaki na Sunday Hyera.
Upande wa mashtaka unawakilishwa na mawakili wa Serikali, Edga Bantulaki na Sunday Hyera.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Frederick Sumaye walihudhuria mahakamani.
Wengine waliofika mahakamani ni mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na wa Viti Maalumu, Devota Minja.
(Habari na Hamida Shariff, Mwananchi )
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )