Jeshi
la Polisi Mkoani Morogoro kwa kushirikiana na Maafisa wa Uhifadhi wa
Wanyamapori wamefanikiwa kumkamata jangili akiwa na meno ya Tembo 5
yenye thamani ya MIL 100 na mshitakiwa yuko kituo cha Polisi morogoro.
Taarifa
kutoka kwa jeshi la Polisi morogoro mshtakiwa anategemea kufikishwa
mahakamani. Aidha, Afisa Habari wa Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori
Tanzania – TAWA Bw. Twaha Twaibu ameeleza kuwa walipata taarifa kutoka
kwa raia wema juu ya kuwepo kwa jangili huyo wa meno na kutuma maafisa
wanyamapori kutoka Makao Makuu ya TAWA wakishirikiana na jeshi la Polisi
na kuweza kumkamata jangili huyo.
Nae
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei akiongelea tukio hilo,
amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo aliejulikana kwa jina la
Nehemiah Nashon akiwa katika chumba namba 104 cha Hoteli ya BZ iliyopo
maeneo ya Nane-nane Mjini Morogoro, na kwamba vipande hivyo vina thamani
ya zaidi ya shilingi Mil. 100.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )