KUNA mchwa ndani ya Serikali ya Rais Jakaya
Kikwete. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Abdulrahman
Ghasia (49) pichani, ni miongoni mwa wanaotafuna fedha za umma serikalini, mithili ya
mchwa. Anaripoti Mwandishi Maalum … (endelea).
Katika kipindi kisichozidi siku 52,
Ghasia ametumia kiasi cha Sh. 25.8 milioni kwa matumizi yake ya simu ya
mkononi, tena kupitia kampuni moja ya Airtel.
Taarifa hizi za
waziri kutumia kiasi cha Sh. 25.8 milioni kwa matumizi ya simu moja ya mkononi,
ndani ya muda usiofikia miezi miwili, zinafichuka katika kipindi ambacho
serikali imekuwa ikitumia nguvu kukusanya michango kutoka kwa wananchi.
Michango mingi
ambayo serikali imekuwa ikikusanya, ni ile ya maabara kwenye shule za kata,
madawati, ununuzi wa vitabu, madaftari na ujenzi wa nyumba za walimu na
madarasa.
Taarifa zinasema,
katika maeneo mengi, maagizo ya serikali, yaliambatana na vitisho, huku baadhi
ya walioshindwa kutoa michango hiyo wakifikishwa mahakamani na kufungwa.
Kwa mujibu wa taarifa
kutoka ndani ya serikali na kampuni ya Aitel Tanzania Limited, waziri Ghasia
ametumia mamilioni hayo ya shilingi kwa mawasiliano kati ya tarehe 1 Februari
na 21 Machi mwaka huu.
“Kuna mambo ya
ajabu sana ndani ya serikali hii. Taifa masikini kama hili, kuna viongozi
wanaotumia kiasi cha Sh. 25 milioni kwa simu. Kwa kweli, umasikini tulionao ni
wa kujitakia,” ameeleza Juma Said, mkaazi wa Kinondoni na mchambuzi wa masuala
ya kisiasa na kijamii.
Nyaraka (Invoice) kutoka Aitel inamuonyesha Ghasia alipewa ankara
ya malipo ya tarehe 1 Februri 2015, yenye Na. 29906000001374, ikielekeza
serikali – Tamisemi – kulipa kwa
kampuni hiyo, jumla ya Sh. 25,878,335.86.
Kwa mujibu wa
nyaraka hizo, Ghasia amejitambulisha kuwa ni waziri wa Tamisemi. Anatumia
anuani ya S.L.P 23, jijini Dar es Salaam; huku namba ya mteja – Customer Id –
ikitajwa kuwa 1219937034.
Ghasia anatumia namba ya mlipa kodi (TIN) TIN: 100-961.520.
C hanzo changu kiliweza
kuripoti kuwa kila mwaka serikali inatumia mabilioni ya shilingi kwa njia za
anasa, ikiwamo malipo ya simu, usafiri, nguo na fenicha za ndani, badala ya
fedha hizo kuwekezwa kwenye maendeleo.
Chanzo ni Mwanahalis.oline
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )