CHANGA! Mkongwe
kwenye sanaa ya vichekesho Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ amejikuta
kwenye wakati mgumu baada ya kutapeliwa shilingi milioni mbili
alizopaswa kulipwa kwenye shoo ya Instagram iliyofanyika hivi karibuni
katika Viwanja vya Posta, jijini Dar.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wiki moja
kabla ya shoo hiyo, mwigizaji Wema Sepetu alimpigia simu Mzee Majuto
aliyekuwa nyumbani kwake mkoani Tanga na kumpa ‘dili’ la kutokelezea
kwenye shoo hiyo (special appearance) kwa maelewano ya malipo ya
shilingi milioni mbili taslimu.
“Mzee Majuto alionekana kwenye shoo hiyo
akiwa kama staa mualikwa akiwa na mchekeshaji mwenzake Stan Bakora
pamoja na Wema mwenyewe ambapo mbali na uwepo wao katika pati hiyo
walitakiwa kufanya kazi kama vile kuchekesha mashabiki wao.
“Baada ya shoo kuisha na kila mtu kula
zake, Mzee Majuto alimuulizia Wema kuhusu mkwanja wake lakini hakupata
majibu yaliyoeleweka wakati wenzake wote wakiwa wameshalipwa chao.
“Wema alishangazwa na ishu hiyo ndipo
alipomtafuta muandaaji wa shoo (Fredy Mgimba ‘Frekon’) lakini aliingia
mitini jambo lililomfanya Wema avujishe siri kwenye ukurasa wake wa
Instagram akidai kuwa waandaaji wa Instagram Party wamemfanya aonekane
vibaya kwa kutomlipa Mzee Majuto fedha zake na kuongeza kuwa hatofanya
nao kazi tena,” kilisema chanzo chetu.
Baada ya kunyaka ubuyu huo kutoka kwa
chanzo chetu, waandishi wetu walianza ‘kumvutia waya’ Mzee Majuto ambaye
alikiri kupewa dili hilo kupitia kwa Wema na kudai waandaaji
‘wamemuingiza mjini’.
“Hao wamenidhulumu kwa kuwa mimi ni mzee
na wamenitumikisha usiku mzima bila kunipa chochote, sawa tu hakuna
shida. Sitakwenda kushitaki popote, namwachia Mungu,” alisema Majuto.
Alipotafutwa muandaaji (Fredy), simu
yake iliita muda mrefu bila kupokelewa na baadaye alipokea na kuomba
apigiwe baada ya muda kidogo kwa kuwa anaendesha gari.
Baada ya nusu saa, mwandishi wetu alimpigia simu kwa nyakati tofauti lakini hakupokea tena.
Baada ya nusu saa, mwandishi wetu alimpigia simu kwa nyakati tofauti lakini hakupokea tena.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )