Mohammed Dewji amesikitishwa kutokana na taarifa zilizotolewa katika mkutano mkuu Simba uliofanyika jana July 31 2016, kuwa yeye ambaye aliomba kununua asilimia 51 ya hisa za Simba kama mfumo ukibadilishwa, hajaandika barua kwa uongozi wala kukutana nao ila amekuwa akiongea kupitia vyombo vya habari kitu ambacho sio kweli.
“Kiukweli nimesikitishwa kwa wanaosema dhamira yangu ya kutaka hisa Simba nimeomba kupitia vyombo vya habari na wala sijaandika barua, ukweli nimekutana na Rais wa Simba Evans Aveva zaidi ya mara tatu, ameshakuja ofisi kwangu zaidi ya mara tatu”
“Kuhusu kuandika barua nilikuwa sijaandika kwa sababu mfumo wa hisa niliokuwa nahitaji ulikuwa haupo sasa utaombaje kitu ambacho hakipo, ila leo baada ya mkutano mkuu kukubali nimeandika barua rasmi kwenda kwa uongozi wa Simba na tayari tumeshaituma”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )