Ilipoishia...
Kwa
kupitia kwenye kiio nikazishuhudia gari sita za polisi zikija katika
eneo ilipo ndege na kuizuia isiondoke na katika kuchungulia vizuri
nikamuona askari lawrance akizungumza na waongozaji wa ndege wa chini
akiwaomba ndege isiondoke na wakihitaji kumshusha mmoja wa abairia wa
ndege hii na kwa haraka nikajua ni mimi ndio wamenifwata na kuyafanya
mapigo yangu ya moyo kuanza kwenda kasi na amani ikanitoweka moyoni
mwangu
Endelea...
Kutokana
tayari injini za ndege zilishaanza kuata moto haikuwa rahisi kwa
kuisimamisha ndege ambayo taratibu ilishaanza kuondoka kuzipisha ndege
nyingine ambazo zinasubiri kutua na kila kitu katika uwanjwa huu wa
ndege vinakwenda na muda wanao jipangia.Macho yangu yakashuhudia jinsi
tunavyo ziacha gari za polisi na ndege inavyo ongeza mwenza na kuitafuta
njia ya kurukia
“ehee mola niokoe mimi mja wako kwa maana mmmm”
Nilijizungumza
kimoyo moyo na kweli ndege ikakaanza kunyanyuka taratibua na kuiacha
ardhi ya afrika kusini hadi ndege inakaa sawa angani ndio nikapata amani
na kajasho taratibu kakanishuka huku kwa mbali nikijasikilizia jinsi
mapigo ya moyo yanavyo punguza kasi yake,safari ikaendelea kwa amani na
kutokana na uchovu mwingi nikajikuta nikilala fofofo pasipo na kitu
kilicho nistua ni kipaza sauti cha rubani akituomba tufunge mikanda yetu
vizuri kwani ndege inajiandaa kutua katika uwanja wa jomo kenyata
nchini kenya
“mmmmmmm”
Nikajikuta
nikiguna kwani sijazoea kuziona ndege zinazo toka nchini afrika kusini
kutua kenya ili kwenda tanzania na isitoshe kwa maelezo niliyo yasikia
wakizungumza mama na balozi wa tanzania ni kwamba ndege inakwenda moja
kwa moja tanzania.Moyo wangu ukaanza kupoteza amani tena ikanilazimu
kumiya muhudumu wa ndege na hakusita kunifwata sehemu nilipo na
kunisikiliza haja yangu niliyo muitia
“sijui nimesikia vibaya au....? Ni kweli tutatu kenya?”
“ndio
kuna mzigo tunaishusha kwanza na pia kuna mmoja wa abiria nanhitajika
kurudisha afrika kusini kwahiyo tunaiwahi ndege ya shirika letu inayo
ondoka kenya saa sita usiku na tutamkabidhi abiria huyo kwa askari.”
Moyo ukawa kama umelipuliwa na bomo,kuzungumza nikajikuta nikishindwa na kubaki nikimtazama muhudumu kama sanamu la kushangaza
“halloo mr”
Nikastuka
na kumtazama muhudumu wa ndege ambaye alikuwa akinipungia mkono mbele
ya uso wangu baada ya kuniona nikiwa nimegandishwa kama sanamu
“umesema kuna mtu anashushwa?”
“ndio hiyo ni taarifa tuliyo powa tukiwa njiani”
“ni mwanume au mwanamke”
“kusema kweli hatujatajiwa ni jinsia gani?”
“nashukuru”
“na wewe pia”
Muhudumu
akaondoka na kuniacha nikitawaliwa na mawazo na laiti ingekuwa nipo
kwenye gari nigeweza kuruka na kufilia mali.Kitu cha ndege ni ngumu sana
kujirusha,rubani akatutangazia kuwa zimesalia dakika tano kwa ndege
kutua na kila mto ahakikishe kuwa amejifunga vizuri mkanda wake hapo
ndipo nikakumbuka na mimi kujifunga mkanda.
Ndani
ya dakika tano ambazo rubadi alisema ndivyo jinsi iliyo kuwa na ndege
nikaanza kushuka chini kwa kasi na matairi yake yakaanza kukanyaga ardhi
ila gafla tukasikia mlio wa ‘kwaaa’ kama kitu kilicho katika na
kuifanya ndege kuegemea upande wangu niliopo na wezangu tulio kaa upande
huu.Milio ya vyuma kukatika katika tukazidi kuisikia na si mimi mwenye
niliye anza kupiga kelele za kumuomba mungu ila hadi wezangu nao
wakafanya hivyo huku kila mmoja akiomba kwa lugha anayo ijua yeye
mwenyewe
Ndege
ikazidi kulala upande wetu na kazidi kuserereka na mbaya zaidi moto
mwingi ukaanza kuwaka sehemu ya nyuma mita chache kutoka ilipo siti
yangu na kunilazimu kuufungua mkanda ili kuyaokoa maisha yangu kama
wanavyofanya wezangu.
Nikawahi
kuishika siti ya mbele yangu ili kujizuia na upepo mwingi unao nivuta
nyuma kutoka katika sehemu ulipo moto ambao umepasua sehemu nzima ya
nyuma.Nikajikaza kwenda mbele na watu walio shidwa kujishikilia
walivutwa nyuma kwenye moto.Kelele na vilio vikazidi kutawala na kila
sehemu na watu wengi wakawa wamebanwa na siti zao kiaisi kwamba baadhi
yao walijigonga vibaya kwenye vyuma na vichwa vyao kupasuka vibaya na
wengine kukatika viungo vya miili yao.
Ndege
ikagonga sehemu na kusababisha mtikisiko mkubwa na kupinduka kichwa
chini miguu juu jambo lililosababisha mikono yangu kushindwa kuhimili
kuishikilia siti niliyo kuwa nimeishika na nikajikuta nikiachia na
kuanza kuvutwa nyuma na upepo mkali uliochanganyika na moto ambao ni
mkali sana,gafla nikastukia nikidakwa mkono na kuangalia vizuri
nikamkuta ni sheila ambaye amenishika mkono huku na yeye akiwa amekaa
kwenye siti yake na kuzuiwa na mkanda alio jifunga na huku mkono mmoja
akiwa ameushika kwenye siti iliyopo pembeni.
Nikamtazama
kwa macho ya huzuni na kumuona akishindwa kuhimili uzito wangu kwani
tegemezi lote la mwili wangu ni mkono wake na sikuwa na sehemu yingine
ya kushikilia
“sheila niachie nife”
“eddy unasemaje?”
“niachie.”
Nilizungumza
huku nikimtazama sheila machoni ambaye anatumia nguvu nyingi kunizuia
nisichomolewe nje ya ndege na mbaya zaidi pembeni yangu hakuna kitu
ambacho ninaweza kusema kuwa nitakishika ili kinizuie nisichomolewe nje
kwani siti zote za nyuma zimechomoka na watu wake.
Ndege
ikaendelea kugonga majengo yaliyopo ya hapa uwanja wa ndege hadi
ikasimama ndipo sheila akaniachia mkono na mimi nikaanguka chini na
kujigonga mkono wangu wa kushoto kwenye upande wa pili wa ndege.Sheila
akaaanza kupata shida ya kujifungua mkanda wa siti yake na mbaya zaidi
kwa jinsi ndege ilivyo anguka imemfanya awe kichwa chini miguu juu
Nikaanza
kusikia ving’ora vya gari za zimamoto zikija katika eneo la tukio na
kuazna kuuzima moto unaoendelea kuiteketeza ndege,moshi mwingi ulio
tawala ndani ya ndege ukanifanya nianza kukohoa na taratibu nikaanza
kujivuta nje ya ndege huku mkono wangu ukitawaliwa na maumivu
makali.Niavutwa nje na waokoaji na gafla mlipuko mkubwa wa ndege
ukatokea na kuturusha mbali mimi pamoja na waokoaji na nikajzidi
kuuegemea mkono wangu ambao ninahisi unamaumivu
“no sheila?”Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
