Mbunge wa Kigoma
Kusini, David Kafulila amekanusha uvumi kuwa ana mpango wa kujiunga na
Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT)-Tanzania,
Kafulila amesema hana
mpango wa kuachana na chama chake na taarifa zilizopo ni za kizushi;
“Hizo taarifa zitaendelea kuwa za tetesi tu, mimi bado mwanachama wa
NCCR-Mageuzi na sina mpango wowote wa kujiunga na chama chochote cha siasa kwa sasa wala kwa baadaye,” David Kafulila.
Mbunge huyo amesema
kwa sasa anaendelea kufanya kazi za jimbo na ana uhakika wa kurudi
bungeni kwa mara nyingine kuwawakilisha wananchi wa Kigoma Kusini
kupitia chama cha NCCR-Mageuzi na si chama kingine cha kisiasa.
Miongoni mwa waliojiunga na chama hicho cha ACT-Tanzania ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Arusha, Samson Mwigamba pamoja na Zitto Kabwe ambao walisimamishwa pamoja na Prof. Kitila Mkumbo, ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.
Wiki iliyopita Mbunge Halima Mdee na John Shibuda, wote wa CHADEMA, walikanusa Bungeni kuhusishwa na mipango ya kujiunga na ACT Tanzania.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )