Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia...
Alizungumza
kwa sauti ya ukali kidogo.Nikiwa ninavua kofia,mkuu wa shule ambaye
tunawindana kama paka na panya naye akawa anaingia ndani ya ukumbi huku
akiwa ameongozana na mkuu wa shule.Akabaki akinitazama kwa hasira na
kuanza kupiga hatua za haraka kunifwa huku mikononi mwake akiwa amekunja
ngumi
Endelea...
Nikaanza
kurudi nyuma huku nikimtazama mkuu wa shule,akazidi kuja kwa kasi
ikanilazimu kusimama nikimtazama kwa umakini.Wanafunzi wote wakawa na
hamu ya kuangalia ni nini ambacho atakifanya mkuu wa shule.Hatua chache
kabla hajanifikia nikaifunua tisheti yangu sehemu ya kiunoni na
kumuonyesha bastola niliyo ichomeka kiunoni.Kidogo akapunguza kasi hadi
ananifikia munkari wote ulimuishia.
“toka katika shule yangu”
Alizungumza
huku meno yake ameyang’ata kwa hasira.Nikamtizama na macho makali na
ukumbi mzima wa shule upo kimya hata kijiko kikianguka mlio wake
utasikika vizuri.
“sitoki”
Wanafunzi wote wakashangilia,mkuu wa shule akawatizama wanafunzi na wakakaa kimya
“walinzi mupo wapi?”
Mkuu
wa shule alizungumza kwa sauti kubwa,hapakuwa na mlinzi hata mmoja
aliye nifwata kila mlinzi aliye niona kuwa ni mimi aliishia mlangoni na
kusimama.Mmiliki wa shule akatufwata sehemu tulipo simama na mkuu wa
shule
“jamani,kuweni wapole.Mkuu unaniambisha bwana”
Mkuu
wa shule akajifanya kama hamsikii muajiri wake,kitu kinacho niumiza
kichwa ni kwanini mkuu wa shule hadi leo yupo wakati amafanya mambo ya
ajabu hadi muda huu hajachukuliwa hatua zozote.Akanisogea katibu
yangu,nikastukia kibao kikali kikitua kwenye shavu langu.Nikataka
kulipiza nikaisikia sauti ya john ikiniita jina langu na nilipo mtizama
nikamkuta john akitingisha kichwa akiniashiria nisifanye chochote
Mkuu
wa shule akanitandika kibao cha pili,ila john akawa na kazi moja ya
kuniomba hadi machozi yakawa yanamwagika,nisilipize chochote kwa mkuu wa
shule.Machozi ya hasira yakaanza kunimwagika,huku kifua changu kikianza
kutanuka kwa hasira kali,akataka kunitandika kofi la tatu nikamdaka
mkono wake.
“nitakuua”
Nilizungumza
kwa sauti ya ukakamavu,huku macho yangu yakimtazama mkuu wa
shule.Akajaribu kuuchomoa mkono wake kutoka kwenye mkono wangu ila
akashindwa.John kwa haraka akaja na kuingia katikati yetu na
kuniachanisha mkono wangu na mkuu wa shule na kunishika mkono na kuanza
kunitoa nje
“eddy achana naye huyo mzee”
Machozi yakazidi kunimwagika,pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote
“john niachie,tafadhali”
“eddy siwezi kukuachia,nakujua.Tuliza kwanza hasira”
“john,yule mzee ananitafuta nini mimi?”
“mpotezee bwana,hajui atendalo”
“john,mama yangu hata siku moja hajawahi kunizalilisha mbele ya watu kwa kunipiga.Sembuse yeye kikaragosi”
“ndio,naelewa hilo eddy ila punguza jazba”
Tukaingia
kwenye moja ya darasa lililopo chini ya ukumbi kwani ukumbi upo
gorofani.John akanikalisha kwenye moja ya kiti na yeye akakaa mbele
yangu juu ya meza.Moyo na mwili wangu vyote vikawa vinajisikia vibaya
sana kwa kitendo cha kuzalilishwa.Kwani katika maisha yangu tangu nikiwa
mtoto sikupenda mtu kunizalilisha wala kunionea.
Hata
awe ni mkubwa vipi nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kupambana naye
hata akinipiga basi ipo siku nitamvizia hata kwa mawe nimpige,ndio maana
hadi hapa nimekua bondia mzuri tuu.Nikaichomoa bastola yangu kwa haraka
john akanibeta na kunipokonya
“eddy,unataka kufanya nini?”
“lete hiyo bastola”
“ahaa eddy sikupi”
John
alikimbia nyuma ya darasa,huku bastola akiwa ameishika
mkononi.Nikamtazama kwa macho makali sana yasiyo pepeseka hata
kidogo.Kwa haraka nikatoka mlangoni na kumfungia john kwa nje.Nikakimbia
na kuanza kupandisha ngazi za kuelekea kwenye ukumbi.Kitendo cha mguu
wangu wa kwanza kukanyaga sakafu ya ukumbini nikatazama wapi alipo mkuu
wa shule.
Nikamuona
akiwa amekaa kwenye meza ya wageni waalikwa akiwa katikati ya waalimu
wengine na mmiliki wa shule.Kwa kasi ya ajabu nikakimbia hadi alipo kaa
na kujirusha na sote wawili tukaanguka na kiti,mbaya zaidi yeye
akangukia mgongo na kunipa mimi nafasi nzuri ya kumkalia kwenye kifua
chake na kuanza kumshambulia kwa ngumi zisizi na idadi kwenye uso wake
Kelele
za wanafunzi kushangilia zikazidi kuongezaka,waalimu walio karibu yetu
wakaanza kunivuta,kuniachanisha na mkuu wa shule.Wakanisimamisha na
kunipeleka pembeni.Mkuu wa shule akasimaa huku akitaka kunifwata ila
waalimu wezake wakanizuia.Ukumbi mzima wanafunzi kuanzia kidato cha
kwanza hadi cha sita wakawa na kazi ya kunishangilia huku wakilitaja
jina langu na kupiga makofi.
“eddy......Eddy........Eddy........Eddy”
Mkuu
wa shule akawazidi nguvu,waalimu walio mshika na kuja kutuvaa na
waalimu ambao wamenishika mimi.Sote tukaanguka chini,kabla mkuu wa shule
hajafanya chochote nikamuwahi kumdaka shingo na kumpiga kabali.Akaanza
kunishindilia ngumi za mbavu,nikamuachia shingo yake na kumsukuma
pembeni na kunyanyuka juu kidogo.Akanyanyuka kwa kasi na kunifwata,kabla
hajanifikia nikaruka juu kwa kutumia mguu wangu wa kulia,nikautulisha
kwenye kifua chake na kumuangusha chini.Waalimu wakaendelea
kutushika,kelele za wanafunzi wezangu zikazidi kuongezeka.Hata ambao
wawanijui vuzuri,nao pia wakawa katika mkombo wa kushangilia
“nitakuua wewe kijana”
Mkuu
wa shule alizungumza huku akiwa ameshikwa na wezake kwa nguvu.Nikabaki
nikitabasamu kwa dharau zaidi nikamnyooshea kidole cha kati kama
tusi.Ndio nikawa nimemfungulia hasira zake zote.Akajibabadua mikononi
mwa waalimu wengine na kunifwata.Nikasikia mwalimu mmoja aliye nishika
akiwaambia wezeke
“hembu muachieni tuone atakacho kifanya,mzee mgomvi kama nini”
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )