Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imetangaza jumla ya
wanafunzi 2679 waliofanikiwa kupata mkopo katika maombi yao ya rufaa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Mikopo, Abdul-RAzaq Badru, ameeleza kuwa kati ya
wanafuzi 4200 waliokata rufaa, wanafunzi 2679 wamefanikiwa kupata mikopo
yao katika mwaka wa masomo 2017/18.
Mkurugenzi
Badru ameeleza kuwa kati ya wanafunzi hao 2769 waliopata mikopo,
wanafunzi 1847 ni wa mwaka wa kwanza ambao mkopo wao umegharimu kiasi
cha shilingi 6.84 bilioni na wanafunzi 832 waliobakia ni wa naoendelea
(mwaka wa 2,3 na 4) ambao mkopo wao umegharimu shilingi 2.75 bilioni.
Hatua
hii ya kuwapangia wanafunzi wapya mikopo inafanya idadi ya wanafunzi
wote wa mwaka wa kwanza walionufaika na mkopo kwa mwaka huu kufikia
33200 ambao mikopo yao ina thamani ya shilingi 108 bilioni.
Aidha
Mkurugenzi Badru ameeleza kuwa tayari Bodi ya Mikopo imeanza kuhamisha
mikopo ya wanafunzi ambao wamebadilisha vyuo na kuwataka wale ambao bado
hawajapata mikopo yao wawe wavumilivu mpaka zoezi la uhamishaji
litakapokamilika.
“Mikopo
ya wanafunzi 590, hii ni mikopo mbayo ilikuwa imeenda vyuo tofauti,
tayari imekwisha kuhamishwa na mikopo hii ina thamani ya shilingi 1.78
bilioni.
"Sasa
hii ndiyo mikopo iliyokuwa imeenda katika vyuo tofauti na tumeanza
kuihamisha kutoka vyuo vile ambavyo wanafunzi hawakwenda ili iwafate
wanafunzi katika vyuo walivyokuwepo na tutaendelea na utaratibu wa
kuhamisha…,” alisema Mkurugenzi Badru.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )