Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi 6 za taasisi za Serikali baada ya
wenyeviti waliokuwepo kumaliza muda wao.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 06 Desemba, 2017 na Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Kwanza Mhe. Rais Magufuli amemteua Bi.
Monica Ngenzi Mbega kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko
kuanzia tarehe 30 Novemba, 2017.
Pili,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Egid Beatus Mubofu kuwa Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) kuanzia tarehe
01 Desemba, 2017.
Tatu,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Abiud Kaswamila kuwa Mwenyekiti wa
Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kuanzia tarehe 01
Desemba, 2017.
Nne,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Esther Hellen Jason kuwa Mwenyekiti
wa Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuanzia tarehe
01 Desemba, 2017.
Tano,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Kenneth Mdadila kuwa Mwenyekiti wa
Bodi ya taasisi ya kifedha ya Self Microfinance Fund Limited kuanzia
tarehe 01 Desemba, 2017.
Sita,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Titus Mlengeya Dismas Kamani kuwa
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania kuanzia tarehe 06
Desemba, 2017.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Desemba, 2017
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )