Mbunge
wa Kibamba, John Mnyika (CHADEMA) amekanusha vikali taarifa
zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amejiuzulu nafasi ya
Naibu Katibu Mkuu Bara ndani ya chama hicho.
Kupitia
mitandao ya kijamii imesambazwa barua inayodaiwa ni ya Mnyika ambayo
imedai kuwa amejiuzulu nafasi hiyo ili aweze kupata muda wa kutosha
kuwatumikia wapiga kura wake.
Mnyika
masema kuwa barua hiyo ni batili na kuwataka wanachama wa CHADEMA na
wananchi kwa ujumla kuipuuza kwani ina lengo la kupotosha umma.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )