Featured
Loading...

HALI YA PELE YAZIDI KUIMARIKA BAADA YA UPASUAJI WA TEZI DUME


AFYA ya aliyekuwa staa wa timu ya taifa ya Brazil, Pele inazidi kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume katika Hospitali ya Albert Einstein mjini Sao Paulo nchini Brazil. 
Hospitali hiyo imeeleza kuwa Pele mwenye umri wa miaka 74 anaendelea vizuri baada ya upasuaji huo uliofanyika wiki hii.
Pele aliwahi kulazwa katika hospitali hiyo takriban miezi sita iliyopita kwa upasuaji wa dharura ili kuondoa mawe katika figo yake.
Pele ambaye jina lake ni Edson Arantes do Nascimento alifunga zaidi ya mabao 1200 wakati alipokuwa akicheza soka na kuisaidia Brazil kushinda mataji matatu ya kombe la dunia.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top