Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, inasemekana ameondoka nchini
Tanzania saa moja baada ya kupatikana taarifa za kupinduliwa kwake na
kiongozi mkuu wa majeshi yake Meja jenerali Godefroid Niyombare
kutangaza kwamba amempindua.
Jenerali huyo mara baada ya tangazo lake, akaweka amri ya kufungwa kwa
kiwanja cha kimataifa cha ndege nchini humo ikiwemo mipaka ya Burundi.
Hata hivyo haiko wazi ikiwa jeshi linamuunga mkono generali Meja
jenerali Godefroid Niyombare.naye msemaji wa rais wa Burundi ,amesema
kwamba wanajeshi watiifu kwa Rais ambaye alikuwa akihudhuria mkutano wa
viongozi nchini Tanzania,amesema nchi iko shwari.
Maelfu ya watu wamekuwa katika shamra shamra katika mji mkuu wan chi
hiyo Bujumbura baada ya wiki kadhaa za maandamano kumpinga katika
maamuzi yake ya kugombea muhula wa tatu wa uongozi,na tayari mpaka sasa
viongozi wakuu wa kanda wamelaani mapinduzi hayo.
Mgogoro wa Burundi umezusha wasi wasi wa kurejea katika ghasia baada ya miaka kumi na miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Zaidi ya watu elfu tatu walikufa katika vita vya kikabila kati ya wahutu
na watutsi ,vita vilivyomalizwa muongo uliopita.na mgogoro wa sasa
nchini humo umehusisha kwa kiasi kikubwa na masuala ya kisiasa.
lakini,yaliyojiri Burundi hayana tofauti na kilichojiri katika nchi
jirani ya Rwanda ambayo ilikumbwa na mauaji ya kimbari nayo ilikabiliwa
na masuala ya ukabila.
Umoja wa mataifa umeonya hivi karibuni kwamba ikiwa ghasia zitasitishwa
Burundi itakuwa na Amani na kama itakuwa vinginevyo basi nchi hiyo
itarejea katika vita vya wenyewe kwa wenyewe .
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )