Ishu hiyo ‘ilidakwa’ na ‘balozi’ wa
gazeti hili usiku wa Jumapili iliyopita ndani ya Ukumbi wa New Maisha,
Masaki jijini Dar kulipokuwa na onesho la Mrs. Mabeste Charity hafla
iliyokusanya mastaa kibao na watoto wengi wa mjini.
Katika pitapita zake huku akikodoa macho kila kona ndani ya ukumbi huo, mwandishi wetu alibahatika kuwaona wawili hao wakiwa wamegandana kwa staili ambayo si ya kujadili katiba mpya huku ukaribu na kutazamana kwao kukiwa na maswali mengi kuliko majibu.

Hata hivyo, umbali wa mkao wao ulianza
kupungua kila dakika moja ilipopita wakawa wanabadili mapozi yakiwemo
kutazamana kimahaba na kushikana kwa kujitawala.
Baada ya kuhakikisha kuwa amepata picha
za ushahidi wa kutosha, mwandishi wetu aliwafuata wawili hao na
kumuuliza Shamsa kama huyo ndiye mbadala wa Nay, akamwambia mwandishi
kuwa haikuwa kazi yake kujua kwani pale walikuwa eneo la starehe hivyo
hawakutaka bughudha na karaha yoyote.
“Ebwana ee, mbona hivyo jamani? Siyo
kazi yako kujua huyu ni nani kwangu, ni msanii mwenzangu na hapa tuko
kwenye sherehe na hatuhitaji usumbufu wowote,” alisema kwa mkato Shamsa.
Kwa upande wake Galis, alisema hana cha kusema kwani hakuwa eneo la mahojiano.
“Kaka huyu ni msanii mwenzangu na hapa si sehemu ya mahojiano,” alijibu.
Nay alipopigiwa simu alisema: “Hawa wanawake wa Bongo Muvi utawaweza! Ila nitadili naye.”

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )