Staa mrembo wa Bongo Movies, Elizabeth
‘Lulu’ Michael amekili kupenda kuwa na mahusiano na ya kimapenzi na
wanaume waliomzidi sana umri.
Akizungumza kwenye The Sporah Show, Lulu amezitaja sababu za kupendelea kutoka na wanaume waliomzidi umri.
SPORAH: Watu wanahisi kwamba Lulu anapenda sana kutembea na watu waliomzidi umri sana,
LULU: That’s true, sio
uongo, sio sana, Napenda kudate mtu ambaye anayeweza kusimama kama
mpenzi, kama kaka, kama baba, kama kiongozi. Sitakuwa tayari kuwa na ile
relation leo tumeamka na Maisha Club, kesho tumeamka na Billicanas,
kesho tumeamka pale tunakula chips, I need to gain from you, nje ya
upenzi unanifundisha nini kwa sababu haimaanishi kwamba mi ntaishi na
wewe milele, itafikia siku labda we utaondoka au mi ntaondoka, we
ukiondoka mi nikibaki nimejifunza nini kutoka kwako na ntaendelea kuishi
vipi.”
“Haimaanishi kwamba napenda kutembea na
watu walionizidi umri labda miaka hamsini, napenda kuwa na mtu ambaye
angalau ananizidi umri, anauzoefu zaidi yangu, amepitia vitu vingi,
anajua vitu vingi kwamba i’ll be there as a girlfriend lakini nakuwa
naiba iba kidogo […] na vitu vingine vya kitoto kitoto vingi vinakuwa
hamna.” alisema Lulu.
Bongo 5
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )