WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Nape Nnauye, amenunua nakala moja ya albamu ya Injili ya msanii
na prodyuza, Goodluck Gozbert, kwa Sh milioni 3 kutokana na kuguswa na
ujumbe uliopo katika albamu hiyo.
Waziri huyo alinunua albamu hiyo wakati
wa uzinduzi wa albamu hiyo ya kwanza ya msanii huyo iliyopewa jina la
‘Ipo Siku’ uliofanyika Mwanza.
“Albamu yangu ilimgusa sana Waziri Nape
Nnauye na yeye kwa kuniunga mkono amenunua nakala moja ya albamu kwa
shilingi milioni 3 na kuamsha ari kwa vingozi wengine waliohudhuria
uzinduzi huo,” alieleza Goodluck.
Albamu hiyo inabebwa na nyimbo ‘Acha
Waambiane’, ‘Hao Hao’, ‘Nimesamehe’, ‘Ndiwe Mungu’, ‘Pendo Langu’, ‘Moyo
Tulia’, ‘Surprise’ na ‘Ipo Siku’ iliyobeba jina la albamu.
Mtanzania
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )