Ambwene
Yessaya ‘AY’, amesema kukithiri kwa matumizi ya dawa za kulevya kwa
wasanii wa muziki wa kizazi kipya nchini kutashusha soko la wasanii hao
kwa kukosa uaminifu.
Akizungumza na gazeti la Mtanzania
Alhamisi hii, AY amesema hizi kashfa za wasanii kutumia madawa ya
kulevya inawachafua wasanii.
“Mimi binafsi nashindwa kuelewa kwanini
wasanii wanajitumbukiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya na huko
tunakoelekea tutashindwa kuaminika kwa jamii, familia zetu hata kwa
watoto na marafiki, inabidi tupigane kwa pamoja, huku tukimshirikisha
Mungu atuepushe na hayo mambo,” alisema AY.
AY aliongeza kwa kuwa muziki wa kizazi
kipya kwa sasa una nafasi kubwa, wasanii watumie fursa hiyo kujiendeleza
kimuziki kwa kushirikiana na wasanii wa mataifa mbalimbali, ili kukuza
uchumi badala ya kushirikiana katika matumizi ya dawa za kulevya.
“Kinachotakiwa kwa sasa, wasanii watumie
fursa za kushirikiana na wasanii wenye mashabki wengi kutoka nje ya
nchi kwa ajili ya kujiongezea mtandao, soko na fedha zaidi, siyo
kujiingiza katika matumizi au uuzaji wa dawa za kulevya,’’ alifafanua AY.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )