H-Baba asema lazima mwanaye aishi kisanii kama wazazi wake,afunguka kuhusu kumuweka 'bleach'
Msanii wa bongo Fleva,H: Baba
amewafungukia mashabiki wake waliomjia juu baada ya kumuweka dawa ya
nywele'bleach' mtoto wake,Tanzanite mwenye umri wa mwaka mmoja.
Mashabiki walimwambia msanii huyo kuwa
bleach siyo nzuri kiafya kwa mtoto huyo,H: Baba akijibu tuhuma hizo
alisema kuwa lazima mwanaye aishi kisanii kama wazazi wake na kwamba
yeye kama mzazi hawezi kumuharibu mtoto wake.
'Watu wanashindwa kuelewa mimi sijampaka
mwanangu bleach hiyo ni hina pia hina ni suna kwa dini yetu ya Kiislam
sioni tatizo hapo,'alisema H: Baba.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )