Takriban
watu 10 wameuawa katika shambulizi la mlipuaji wa kujitolea muhanga
katika msikiti mmoja wa Shia mkoa wa mashariki wa taifa la Saudi Arabia
,kulingana na daktari mmoja.
Daktari wa kukabiliana na dharura
katika hospitali ya Qatif amesema kuwa takriban watu sabini wamejeruhiwa
huku wengine wakijeruhiwa vibaya.Walioshuhudia wameripoti mlipuko mkubwa katika msikiti wa Imam Ali uliopo katika kijiji cha al-Qadeeh,katika jimbo la Qatif.
Kundi la Islamic State limedaiwa kutekeleza shambulizi kama hilo katika taifa jirani la Yemen siku ya ijumaa ambalo liliwajeruhiwa watu kadhaa.
Hatahivyo halijatoa tamko lolote kuhusu sha
Miili iliozibwa na nguo ilionekana imetapakaa katika sakafu ya msikiti huo.
Watu wa dhehebu la Shia walio wachache wanaishi mkoa wa mashariki na kumekuwa na malalamishi ya washia wanaotaka kupewa haki zaidi.
Tukio hilo linajiri huku muungano wa majeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ukiendeleza kampeni yake dhidi ya waasi wa kishia katika taifa jirani la Yemen.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )