Dudubaya amesema haya kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa
Radio alipokuwa akiwaelezea watu aina za maskani zilizopo na kusema kuwa
zipo maskani zingine ni mbovu kwa kuwa zibapoteza watu na kuharibu watu
na kudai kuwa zipo maskani zingine ni endelevu kwani watu
wanabadilishana mawazo kuhusu mambo fulani na kusaidiana mawazo pia.
Dudubaya amewachana baadhi ya mashabiki ambao kupitia kipindi cha eNEWS
walisema kuwa Dudubaya saizi amepoteza njia na muda mwingi amekuwa ni
mtu wa kushinda vijiweni, ndipo hapo aliposema kuwa mashabiki hao kwanza
ni wanafiki na mamluki, ambao wanalengo la kutaka kumchafua adai ni
watu wasiomjua vizuri ambao wametumwa.
"Hao mashabiki ni mamluki tena ni kenge tu hao na mimi nitaendelea kuwa
mamba, hawa jamaa hawajui maana ya maskani wanapaswa kuelewa kuna
maskani potofu ambazo watu hawakuwa machangudoa lakini wanafundishwa na
wanakuwa machangudoa, kuna maskani ambazo watu wanafundishana wizi,
lakini wanapaswa kutambua zipo maskani zingine ni endelevu watu
mnasaidiana na kubadilishana mawazo kutokana na fani zao hata kina
Lowassa na Mbowe wana maskani zao, wanamichezo wana maskani zao hata
sisi wanamuziki wana maskani hata idea za ngoma zangu zote zinatoka
maskani, muziki wa Juma Nature unatoka maskani, hivyo sitaacha kukaa
maskani ili mradi maskani yangu ya watu timamu ambao wanajua majukumu
yao, lakini pia wanapaswa kutambua mimi sishindi kijiweni toka asubuhi
mpaka jioni nakwenda maskani jioni baada ya kumaliza mishe zangu."
Alisema Dudubaya.
Dudubaya aliongezea na kusema msanii kuwa kimya si kigezo cha kufulia
kwani wengine wanatumia muda huo kwenda shule kufanya mambo mengine ya
msingi au wengine wapo kwenye biashara zao, hivyo msanii kukaa kimya
haina maana kuwa amefulia.
"Saizi kama unavyoona King Crazy GK yupo kimya kwa muda kwenye game
lakini juzi juzi hapa amemaliza chuo na sasa ana Masters yake yupo kimya
kimuziki sababu kuna jambo alikuwa anafanya la msingi, na kama
unavyojua mashabiki zetu hawa wanasema kila siku kuwa wasanii wa
Tanzania hawana elimu, lakini tena ukifanya maamuzi hayo labda kurudi
shule wanasema umefulia sijui wanataka nini mashabiki hawa" Alisema
Dudubaya.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )