Baada ya hivi karibuni kukiri kanisani kuwa ameokoka na kumkubali Mungu kuwa bwana na mwokozi wake kisha kukengeuka na kupiga picha chafu za nusu utupu, waumini wamemlipua staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ (pichani akiwa na biblia) kwa madai kuwa anatia aibu.
TUJIUNGE KANISA LA MAKUTI-KAWE
Mara baada ya kushinda Tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Filamu Afrika Mashariki nchini Nigeria mapema mwaka huu kupitia Filamu ya Mapenzi ya Mungu, Lulu alihudhuria ibada kwenye Kanisa la Living Water Centre (Makuti-Kawe) la Apostle Onesmo Nyakura Ndegi lililopo maeneo ya Mahakama ya Zamani, Kawe jijini Dar, kisha akatoa sadaka ya shukrani kwa Mungu aliyemwezesha kutwaa tuzo hiyo.

Mbali
na sadaka hiyo, Lulu akiwa kanisani hapo, aliombewa na kufungukia
kuokoka, jambo lililoibua shangwe kubwa za kumrudishia Mungu sifa na
utukufu miongoni mwa waumini wa kanisa hilo.
TAMKO LA LULU
Katika tamko lake baada ya zoezi hilo kanisani hapo, Lulu alisema:
“Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu pamoja na baba yangu (Michael Kimemeta) na mama yangu (Lucresia Karugila).

“Sijutii kuokoka kwangu na hata wakisema vyovyote I don’t care (mimi sijali) ilimradi namuomba Mungu na mambo yangu yanaenda.”
…..Akiwa na biblia.
KILICHOFUATIA SASA
Mapema wiki hii, Lulu aliibua mjadala mzito miongoni mwa baadhi ya waumini hao wanaotumia mitandao ya kijamii na wale waliokutwa na Ijumaa kanisani hapo kufuatia picha zake chafu za nusu utupu alizoziachia mitandaoni baada ya kuzipiga ufukweni zikimuonesha akiwa amevaa nguo za ndani za bikini na sidiria huku sehemu kubwa ya maungo yake nyeti ikiwa wazi.

PICHA ZAIBUA GUMZO KANISANI
Kwa mujibu wa waumini hao wa Makuti-Kawe, picha hizo ziliibua gumzo kubwa kanisani hapo wakistaajibishwa na kitendo alichokifanya Lulu ambacho ni kinyume na maadili ya kanisa.
“Kiukweli jambo alilolifanya Lulu ni aibu, wakati mwingine tunashindwa kukubali pale anaposema ameokoka kutokana na matendo yake, anastahili kukemewa ili aache mara moja na akae kwenye mstari wa ulokole.

“Kwanza
hapa kwetu hakuna muumini mlokole anayethubutu kupiga picha za ajabu
kama hizo maana ni kinyume kabisa na kanisa letu,” alisema mmoja wa
waumini hao akiungwa mkono na wenzake waliokuwa wakizungumza na gazeti
hili ndani ya viunga vya kanisa hilo.
“Kwanza Mtume Ndegi kama ameziona au akioneshwa zitamsikitisha sana maana ni mtu anayesisitiza usafi wa mioyo na mwili,” alisema muumini mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Jonas na kuongeza:

“Itabidi
kama Lulu atafika kanisani Jumapili (ijayo) aitwe ili aombewe maana
inawezekana alipitiwa na shetani anayetakiwa kukemewa kwa nguvu zote.
LULU ATOA UTETEZI WA KUSHANGAZA
Kufuatia ishu hiyo kuwa kubwa kanisani hapo, Ijumaa lilimtafuta Lulu na kumsomea ‘mashtaka’ yake ambaye alipopatikana alielezwa hoja za waumini kuwa alichokifanya ni kinyume na maadili ambapo katika hali ya kushangaza, hakuonesha kushtushwa na kudai hakuna tatizo kwa kuwa hajapiga kanisani.
“Kwani cha ajabu ni nini hapo? Kwani wameona hizo picha nimepiga kanisani? Kama mnaona hapo ni kanisani sawa, labda ningekuwa nimepiga kanisani lakini sivyo,” alisema Lulu kwa kifupi kisha akakata simu.

MTUME NDEGI ASAKWA
Baada ya kutoridhishwa na majibu ya Lulu yaliyojaa viulizo, gazeti hili lilifanya juhudi za kumtafuta Apostle (Mtume) Ndegi wa kanisa hilo ili kumsikia anazungumziaje suala hilo?
Hata hivyo, juhudi hizo ziligonga mwamba, badala yake simu yake ilipokelewa na mmoja wa wasaidizi wake (jina lipo) na kufunguka kuwa, kitendo alichofanya Lulu si sawa lakini atabadilika neno litakapomkolea.

“Ni
kweli Lulu ameokoka japokuwa siyo moja kwa moja kama inavyopaswa, kwa
sababu mara kwa mara huwa anahudhuria ibada hapa kanisani, lakini cha
kustaajabisha anakuja huku kisha anaenda kufanya hayo mambo yake ya
ajabu, jambo ambalo halitupendezi hata kidogo.
“Ila
sisi hatuwezi kumlazimisha mtu kukaa kwenye mstari kutokana na mambo
yake binafsi kwani siku hadi siku anavyozidi kuja kwenye ibada neno
linavyozidi kumkolea mtashangaa amebadilika kabisa na kuacha yote hayo,
tunaamini hivyo,” alisema mtumishi huyo akiomba kutotajwa gazetini kwani
hana mamlaka hiyo.
SI MARA YA KWANZA KWA LULU KUOKOKA
Tangazo la sasa la kuokoka la Lulu si la mara ya kwanza kwani aliwahi kufanya hivyo baada ya kukutwa na mkasa wa kifo cha aliyekuwa staa wa sinema za Kibongo, Steven Kanumba ambaye pia alikuwa mwandani wake
-Chanzo: GPL

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )