Mwanaume mmoja nchini India amewaua watu 14 wa familia yake kwa kuwachoma na kisu wakiwa wamelala, 2 kati yao walikuwa wazazi wake.
Saba kati ya waliouawa ni watoto
Polisi wasema kuwa waliitwa katika nyumba moja katika kijiji cha Thane, karibu na Mumbai na majirani waliomsikia mwanamke akipiga kelele akitaka asaidiwe.
Mwanamke huyo, ambaye ni dada ya muuaji, alikuwa wa pekee katika familia hiyo kunusurika mauaji hayo ya kikatili.
Maafisa wa upelelezi wanasema inawezekana kuwa mtu huyo alifunga milango yote kwa ndani kabla ya kuwaua jamaa zake.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )