Ali Kiba
Akizungumza katika kipindi cha The playlist cha Times Fm, Kiba amesema hakuwahi kufanya nao kazi ndio maana ana hamu nao sana.
“Kiukweli Master Jay na P funk natamani sana kupiga nao kazi, na naahidi kuwatafuta na kufanya nao kazi, kwa hiyo fans wangu wategemee kazi nzuri ntakazofanya nao” alisema.
Katika ‘line’ nyingine King kiba amedai, anamkumbuka sana pia producer aliyetengeneza kazi zake kadhaa, KGT kwa sababu alikuwa ni zaidi ya mwalimu wa muziki kwake.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )