Meneja wa lebel ya WCB Babu Tale ametoa
fursa kwa wasanii wa kike wenye vipaji kuonyesha vipaji vyao, na
hatimaye kuweza kupata fursa ya kuwa chini ya uongozi wao wa WCB.
Babu Tale ametoa fursa hiyo alipokuwa
akiongea ndani ya Planet Bongo ya East Africa Radio, alipoenda
kumtambulisha msanii mpya amabye atakuwa chini ya uongozi huo Raymond
TipTop, na kusema kuwa wasani wa kike ni wachche hivyo wana fursa kubwa
ya kufanya vizuri iwapo watajituma.
Tuna Plan kuwapata wasanii wa kike
lakini wenye vipaji vya ukweli, asikwambie mtu industry yetu ina
wanawake wachache, tungepata wananwake wanne hata watano', alisema Babu
Tale
Pia babu Tale alisema anatamani sana
msanii Ruby angekuwa kwenye management yake, kwani ana uwezo mkubwa
lakini kwa bahati mbaya ytayari yuko chini ya management nyingine ya
THT.
Kwangu mimi ingekuwa Ruby hayuko chini
ya THT, au hana management tungemchukua, lakini nasema hivi, kama
anakuja mwanamke, awe na level ya kufanana na Ruby au kumshinda Ruby",
alisema Babu Tale
Pamoja na hayo nae Diamond Platnums
amesema ameweka wazi vigezo ambavyo msanii huyo wa kike avifikie ili
aweze kuwa chini ya uongozi huo, pamoja na kujituma tofauti na
walivyozoea kuwa hawawezi.
Aweze kuandika mashairi, aandike nyimbo
zake mwenyewe unajua kuna kitu kimoja, wanawake washajiwekea kuwa wao
hawawezi, sio kweli hawataki kufocus na kujaribu", alisema Diamond.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )