Meneja wa Yamoto Band na TMK Wanaume Family Said Fella ‘Mkubwa Fella’ anajipanga kuogombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2040 akiwa na umri wa miaka 60.
Fella
ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kilungule wilayani Temeke jijini Dar es
salaam (CCM), amekiambia kipindi cha Enewz cha East Africa Television
Jumatano hii kuwa yeye ni mtu makini, hivyo hawezi kushindwa kuiongoza nchi.
“Kama
Mungu akinipa uhai mwaka huo nitakuwa na miaka 60 na nitakuwa nina
uelewa wa kutosha na uwezo wa kuweza kuwaongoza watanzania kwa kujali
maslahi yao ili kuwawezesha kujikwamua na umaskini” Alisema Fella.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )