JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/9 11 Machi, 2016
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 188 kwa ajili ya Wizara, Taasisi zinazojitegemea na mamlaka za Serikali za Mitaa kama inavyoonyesha hapa chini.
1.0 MHANDISI NISHATI II NAFASI 5 (LINARUDIWA)
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kuratibu miradi ya nishati katika ngazi zote,
• Kufuatilia maendeleo ya teknolojia mbalimbali na matokeo ya uvumbuzi na utafiti katika fani zao
• Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu matumizi bora ya nishati kutokana na maendeleo ya teknolojia,
• Kufanya ukaguzi wa shughuri za nishati ikiwa ni pamoja na kuhakiki viwango vya ubora wa huduma za nishati zitolewazo, uingizaji wa petrol na utunzaji wa nishati,
• Kusimamia utendaji wa kazi wa wahandisi nishati waliopo chini yake.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Shahada/Stashahada ya juu ya Uhandisi wa Nishati (Energy Engineer) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.
1.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
=========
2.0 MHANDISI MITAMBO II MKUFUNZI (METAL TECHNOLOGY) (LINARUDIWA) NAFASI - 1
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Wahandisi hawa watafanya kazi ya kufundisha somo la Ufundi Mitambo katika vyuo vya maendeleo ya Jamii Tanzania Bara
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufundisha somo la ufundi mitambo katika vyuo vya Maendeleo ya Jamii.
• Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo
• Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
• Kutunza vifaa vya kujifunzia na kufundishia
• Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti
• Kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu somo la uhandisi maji.
• Kutunga na kusahihisha Mitihani ya wanachuo.
• Kufanya utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbalimbali
• katika jamii inayozunguka chuo
• Kutoa ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha sita waliofuzu Mafunzo ya Shahada/ stashahada ya juu katika fani ya Uhandisi Mitambo (Metal Technology) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
2.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
==========
3.0 MKUFUNZI MSAIDIZI DARAJA LA II –HOME ECONOMICS/ DOMESTIC SCIENCE (LINARUDIWA)- (NAFASI 6)
• Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto. Wakufunzi wasaidizi hawa watafanya kazi ya kufundisha somo la ushonaji, ufumaji, kudarizi, upishi na lishe katika vyuo vya maendeleo ya wananchi Tanzania Bara
3.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufundisha masomo ya ushonaji, ufumaji, kudarizi na upishi na lishe katika vyuo vya maendeleo ya wananchi.
• Kutayarisha mpango wa kazi wa Mafunzo
• Kupima Maendeleo ya Wanachuo katika nadharia na vitendo
• Kutunza vifaa vya kufundishia
• Kufanya na kutoa taarifa za Utafiti
• Kutoa Ushauri wa kitaalam
• Kuandaaa kanuni na taratibu za kusimamia Mitihani chuoni
• Kutunga na kusahihisha Mitihani
• Kufanya Utafiti utakosaidia kutoa majibu kwa matatizo/changamoto mbalimbali katika jamii inayoizunguka chuo
• Kutoa Ushauri juu ya kuboresha Taaluma chuoni na kuendeleza Mafunzo nje ya chuo
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu mafunzo ya stashahada ya ufundi katika fani za ushonaji, ufumaji, kudarizi, upishi na lishe kutoka vyuo vya ufundi vinanvyotambuliwa na Serikali.
3.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
=========
4.0 MUUNDA BOTI DARAJA II (BOAT BUILDER II) – NAFASI 3
4.1 MAJUKUMU YA KAZI (LINARUDIWA )
• Kusaidia kuunda boti za uvuvi
• Kuwashauri wavuvi juu ya utunzaji na matumizi ya boti
• Kufanya matengenezo ya boti.
• Kusaidia kutafsiri/kusoma michoro ya kiufundi ya boti.
• Kuandaa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa boti.
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye stashahada ya Uundaji boti kutoka chuo cha Mbegani au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
4.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi
============
5.0 DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) – NAFASI 31
5.1 MAJUKUMU YA KAZI (LINARUDIWA)
• Kuendesha magari ya abiria, magari madogo na malori
• Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo,
• Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,
• Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C” ya uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua miaka mitatu bila kusababisha ajali na wenye Cheti cha Majaribio ya ufundi Daraja la II (Trade test II).
5.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS. A kwa mwezi.
6.0 MPISHI DARAJA LA II (COOK II ) NAFASI – 7(LINARUDIWA)
• Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Wapishi hawa watafanya kazi ya kuwapikia wanachuo katika vyuo vya maendeleo ya wananchi
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kuandaa chakula cha wanachuo kulingana na Menyu na idadi ya wanachuo
• Kupika chakula cha wanachuo
• Kutoa ushauri kwa uongozi wa chuo kuhusu chakula cha wanachuo.
• Kusimamia jiko.
6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne/sita waliofuzu mafunzo ya cheti yasiyopungua mwaka mmoja katika moja ya fani ya “food Production” yatolewayo na vyuo vya Forodhani (Dar es Salaam),Masoka (Moshi), Arusha Hotel, Y.M.C.A (Moshi), VETA (mikumi) na Vision Hotel (Dar es Salaam) kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali.
6.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGSC kwa mwezi.
===========
7.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI– NAFASI 30 (LINARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
• Kufunga mfumo wa umeme unaohitajika kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
• Kufunga mota na vifaa vingine vya umeme vya aina mbalimbali vya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
• Kufanya usafi na ukaguzi wa mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine vya umeme na miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu wa pampu na kuzuia uharibifu;
• Kuendesha mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
• Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na ya kuzuia uharibifu kwenye mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine umeme kwa kufuata miongozo ya uendeshaji, na inapohitajika kwa dharura.
• Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
• Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali ambao wana Cheti cha ufundi Daraja III (Plants Technician Electrical).
7.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
========
8.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI - (ASSISTANT TECHNICIAN WELDING) NAFASI 4 (LINARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
• Kufunga pampu na injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
• Kufanya usafi na ukaguzi wa pampu na injini za miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
• Kuhudumia uendeshaji wa pampu na injini za miradi ya maji;
• Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi nay a kuzuia uharibifu wa pampu na injini kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
• Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya pampu na injini za miradi ya maji;
• Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali ambao wana Cheti cha ufundi Daraja III katika fani ya Welding na fiter turner.
8.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
9.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI ( UJENZI – CIVIL TECHNICIAN ) – NAFASI 27 (LINARUDIWA)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga.
9.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufanya kazi za ujenzi wa kuta za nyumba na kupaka rangi na kufunga mabomba,
• Kuchonga vifaa vya nyumba za serikali ikiwa ni pamoja na samani “furniture”,
• Kufanya kazi za upimaji (Survey) wa barabara, majengo na mifereji kama atakavyoelekezwa,
9.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa waliomaliza kidato cha IV katika masomo ya Sayansi na kufuzu mafunzo ya mwaka mmoja katika Fani ya Ufundi wa Ujenzi (Civil Technician) kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali,
Au
• Kuajiriwa waliomaliza kidato cha IV wenye cheti cha Majaribio ya ufundi hatua ya II (Civil Technician) kutoka chuo cha ufundi katika mojawapo ya fani za ufundi Ujenzi.
9.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
.
===========
10.0 DOBI DARAJA LA II – NAFASI 1 (LINARUDIWA)
10.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufanya uchambuzi wa nguo kwa ajili ya kuosha, kukausha, kunyoosha na kuzifungasha.
10.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofuzu mafunzo ya miaka miwili au mitatu katika fani ya Dobi (Laundry Services) kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
10.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS. C kwa mwezi.
=========
11.0 MPOKEZI (RECEPTIONIST) – NAFASI 3 (LINARUDIWA)
11.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kupokea wageni na kuwasaili shida zao.
• Kutunza rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya uchambuzi wa wageni wanaoingia ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni.
• Kupokea na kusambaza maombi ya simu za ndani.
• Kutunza na kudumisha usafi wa “Switchboard” na ofisi zake.
• Kuwaelekeza wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi watakakopewa huduma.
• Kuhakikisha kwamba wageni wanaoingia ndani wanamiadi (Appointment) au wamepata idhini ya maafisa husika.
• Kupokea simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maofisa mbalimbali ofisini.
• Kupokea simu kutoka “Extension” za ndani na kupiga nje ya ofisi.
• Kutunza rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka nje ya ofisi na zinazopigwa kwenda nje.
11.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV waliofaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati na kufuzu mafunzo ya Mapokezi na Upokeaji Simu kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
11.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi
============
12.0 MTUNZA BUSTANI DARAJA LA II - NAFASI 3 (LINARUDIWA)
12.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kupanda maua katika maeneo yanayohusika.
• Kupanda na kukata majani na kumwagilia maji.
• Kupanda mboga, matunda katika bustani.
• Kupalilia mazao katika bustani.
• Kufanya kazi zingine zitakazoelekezwa na Viongozi wa Kitengo chao.
12.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye Cheti katika fani ya utunzaji bustani za maua, mboga na upandaji majani kutoka chuo cha Maendeleo ya Wananchi, VETA, au JKT au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
12.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
===========
13.0 AFISA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II (BEEKEEPING OFFICER II) – NAFASI- 5
13.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na manzuki.
• Kutangaza Sera na Sheria za ufugaji nyuki.
• Kufundisha masomo ya fani ya ufugaji nyuki.
• Kukusanya takwimu za rasilimali na ufugaji nyuki.
• Kupanga na kupima ubora wa mazao ya nyuki.
13.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye Shahada katika fani ya Ufugaji Nyuki au Sayansi ya Elimu ya Mimea, Elimu ya Wadudu au Elimu ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
13.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
=========
14.0 MFUGAJI NYUKI MSAIDIZI DARAJI LA II – NAFASI – 5
14.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kusimamia manzuki.
• Kutunza hifadhi za nyuki.
• Kukusanya takwimu za ufugaji nyuki.
• Kutunza kumbukumbu za kazi za utafiti.
• Kuondoa nyuki wanaodhuru binadamu na mifugo.
• Kutoa leseni za biashara ya mazao ya nyuki.
• Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wananchi juu ya ufugaji endelevu wa nyuki na matumizi bora ya mazao ya nyuki.
• Kutunza makundi ya nyuki wanaouma na wasiouma.
14.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha Nne au Sita wenye Astashahada (Cheti) au Stashahada (Diploma) ya Ufugaji Nyuki kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
14.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B na TGS kwa mwezi.
============
15.0 MPIGA CHAPA DARAJA LA II (PRINTER GRADE II) – NAFASI 7
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Ofisi ya Waziri Mkuu
15.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufuatilia utekelezaji wa kazi zinazoendelea na kutoa taarifa kwa msimamizi wa kazi
• Kutayarisha vielelezo (job jacket lay out) kuhusu mtiririko wa kazi (Plan of Production)
• Kupanga ratiba ya kazi
• Kuandaa vifaa vya kufanyia kazi
• Kugawa kazi kwa watumishi walio chini yake
15.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye Stashahada(Diploma) ya kawaida ya Kupiga Chapa,kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
===========
16.0 MPIGA CHAPA MSAIDIZI (ASSISTANT PRINTER) - NAFASI 10
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu.
16.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kukunja karatasi ngumu na kutengeneza „covers‟ za vitabu, majarida, madaftari katika mahitaji mbalimbali kwa kugandisha, kuweka pamoja au kushona katika hali mbalimbali za ubora.
• Kukarabati vitabu, kumbukumbu mbalimbali au majarida kwa kuyawekea gamba jipya, au kurudisha katika hali yake ya mwanzo kutegemea na kifaa hicho kilivyoharibika.
• Kupanga vifaa vilivyotengenezwa katika makasha kwa vipimo vyake au katika seti.
• Kuendesha mashine za kukata karatasi/kupiga Chapa/Mashine za Composing, kushona au kugandisha vitabu, majarida, madaftari na vifaa vingine vinavyokuwa vimetakiwa kwa mtindo na ubora wake.
• Kupanga karatasi zitakazochapwa kwa hesabu ya kila kitabu, jarida, daftari na vinginevyo kwa kushonwa au kugandishwa pamoja.
16.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV au VI katika masomo ya Sayansi, au Sanaa, wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la I (Trade Test Grade I) katika Lithography/Composing/Binding/Machine Minding, au waliohitimu mafunzo ya miaka miwili ya Kupiga Chapa.
16.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.Bkwa mwezi
=========
17.0 MHANDISI II MITAMBO I (MECHANICAL ENGINEER) – NAFASI 5
17.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufanya kazi chini ya uangalizi wa Mhandisi aliyesajiliwa na bodi ya usajili wa Wahandisi kama Professional Engineer ili kupata uzofu unaotakiwa.
• Kufanya kazi kwa vitendo katika fani ya Mekanika ili kumwezesha kupata sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi.
• Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu magari na mitambo mbalimbali, bei za magari na mitambo na vifaa vya umeme ndani na nje ya nchi.
• Kupitia mapendekezo ya miradi (project proposals) mbalimbali ya Ufundi .
17.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya Uhandisi (Mechanical Engineering) kutoka vyuo vikuu vinavyotambulika na Serikali.
17.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
========
18.0 24
19.0 BI DARAJA LA II – NAFASI 1
19.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kupanga ratiba ya kazi kwa watumishi walio chini yake
• • Kuhakikisha kuwa maktaba ni safi
• Kufanya kazi nyingine za maktaba atakazopangiwa na Mkuu wa kituo
19.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza katika fani ya ukutubi au sifa inayolingana na hiyo kutoka katika vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali
19.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
20.0 AFISA MISITU DARAJA LA II (FORESTRY OFFICER GRADE II) –NAFASI- 1
20.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kusimamia upandaji na uhudumiaji wa miti na misitu.
• Kusimamia uendelezaji wa misitu ya kupandwa isiyozidi hekta 5,000 au ya asili isiyozidi hekta 10,000.
• Kufanya utafiti wa misitu.
• Kutekeleza Sera na Sheria za misitu.
• Kuendesha mafunzo ya Wasaidizi Misitu.
• Kukusanya takwimu za misitu.
• Kufanya ukaguzi wa misitu.
• Kupanga na kupima madaraja ya mbao.
• Kudhibiti leseni na uvunaji wa miti.
• Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi endelevu ya miti kwa wananchi.
• Kufanya ukadiriaji wa rasilimali za misitu.
• Kupima maeneo na kuchora ramani za misitu.
20.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye Shahada ya Misitu kutoka chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine au Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
20.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
==========
21.0 MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA II – NAFASI- 5
21.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi na mbuga za wanyamapori.
• Kusimamia utekelezaji wa taratibu za uwindaji na utalii.
• Kutekeleza kazi za maendeleo katika Mapori ya Akiba.
• Kuhakiki ulinzi wa nyara za Serikali.
• Kuhakiki vifaa vya doria.
• Kudhibiti usafirishaji wa wanyamapori na nyara nje na ndani ya nchi.
• Kudhibiti matumizi ya magari ya doria.
• Kuratibu uingiaji wa wageni katika Mapori ya Akiba.
• Kusimamia uwindaji wa kitalii.
• Kudhibiti na kusimamia umilikaji wa nyara.
• Kuweka mikakati ya kudhibiti moto mkali.
• Kukusanya takwimu za wanyamapori na mimea.
21.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au Kidato cha VI, wenye stashahada ya Uhifadhi wa Wanyamapori Mweka au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
21.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B na C kwa mwezi.
===========
22.0 AFISA UGAVI MSAIDIZI II (ASSISTANT SUPPLIES OFFICER) – NAFASI 1
22.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kutunza ghala la vifaa lenye thamani ndogo.
• Kupokea vifaa vipya vitakavyoletwa na wazabuni mbalimbli na kupokea vifaa ambavyo vimetumika lakini vinahitaji kutunzwa kabla ya kufutwa.
• Kufungua na kutunza “Bin Card” kwa kila kifaa kilichopo ghalani.
• Kufungua “Ledger” ambayo itatunza kumbukumbu ya vifaa vinavyoingia, kutunzwa na kutoka kwa nyaraka mbalimbali.
• Kutoa vifaa kwa wateja na watumiaji wengine.
• Kuhakikisha kwamba ghala na vifaa vilivyomo vinatunzwa katika hali ya usafi na kwa usalama.
• Kuandaa hati za kupokelea vifaa.
• Kufanya kazi zingine atakazopangiwa.
22.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye cheti cha “National Store-Keeping Certificate au “Foundation Certificate” kitolewacho na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa au wenye Cheti kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.
22.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.A kwa mwezi
===========
23.0 MSAIDIZI WA OFISI – NAFASI- 10
23.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na ndani ikiwa ni pamoja na kufagia, kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani, kupalilia bustani, kumwagilia maji bustani, kupanda maua au miti na kusafisha vyoo.
• Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine kwsa maofsa waoaohusika na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
• Kusambaza barua za Ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa.
• Kutayarisha chai ya ofisi.
• Kupeleka mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka Posta.
• Kuhakikisha kwamba vifaa vya ofisi vinaweka sehemu zinastahili.
• Kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati wa Asubuhi na Jioni kuyafunga baada ya Saa za Kazi.
• Kudurufu barua au machapisho kwenye mashine za kudurufia.
• Kuweka katika majalada nakala za barua zilizochapwa katika ofisi walizomo.
• Kutunza vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika.
23.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu vizuri katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.
23.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A
===========
24.0 MLINZI - NAFASI- 5
24.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kuhakikisha kwamba mali yoyote ya ofisi inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina hati ya idhini.
• Kuhahikisha kuwa mali yote inayoingizwa langoni inazo hati za uhalali wake.
• Kulinda usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku.
• Kuhakikisha kwamba milango na madirisha yote yamefungwa ipasavyo mwisho wa saa za kazi.
• Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia katika eneo la ofisi wana idhini ya kufanya hivyo.
• Kupambana na majanga yoyote yatakayotokea katika sehemu ya kazi kama vile, moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika kama vile, moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika.
• Kutoa ushauri wa jinsi ya kuboresha huduma ya ulinzi mahali pa kazi.
24.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne waliofuzu mafunzo ya mgambo/polisi/JKT au Mafunzo ya Zimamoto kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.
24.3 MSHAHARA
• Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A
==========
25.0 BARAZA LA SANAA LA TAIFA (BASATA)
Baraza la Sanaa la Taifa ni shirika la Umma lililoundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya mwaka 1984. (Sheria ya kuunda upya Baraza la Sanaa la Taifa kwa kuunganisha Baraza la Sanaa la Taifa na Baraza la Muziki la Taifa na kufuta Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa ya mwaka 1974 na Sheria ya Baraza la Muziki la Taifa ya mwaka 1974 na kuweka utaratibu kuhusiana na mambo hayo. Kazi za Baraza la Sanaa la Taifa ni Kufufua, kukuza na kuendeleza kazi za sanaa ikiwa ni pamoja na Uhamasishaji, Usimamizi, Uimarishaji, Uratibu, Utafiti, na Ushauri wa kazi mbalimbali za Sanaa.
25.1 MKURUGENZI WA UTAFITI NA UKUZAJI WA STADI ZA WASANII – NAFASI - 1 (LINARUDIWA)
25.1.1 MAJUKUMU YA KAZI
• Kuongoza Idara ya Utafiti na ukuzaji wa stadi za Sanaa.
• Kuandaa mpango wa Utafiti na kusimamia utekelezaji.
• Kuandaa mpango wa kukuza stadi za wasanii na kusimamia utekelezaji.
• Kuwasiliana na watafiti mbalimbali na kushirikiana nao.
• Kuandaa na kusimamia makubaliano na watafiti wanaojiajiri kwa muda kufanya tafiti maalum
• Kubaini na kuteua wawezeshaji wa ukuzaji wa stadi za wasanii.
• Kusimamia uchapishaji wa majarida na vitabu vya Baraza.
25.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
• Kuajiriwa wenye Shahada ya Uzamili katika fani za Sanaa (Master of Arts in either Performing Arts, Theater Arts or Cultural and Heritage kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
• Uzoefu wa kazi usiopungua miaka nane (8) ambapo miaka mitano (5) kati ya hiyo ikiwa ni kwenye nafasi ya uongozi katika idara mbalimbali zilizo chini ya taasisi za umma.
25.1.3 MSHAHARA
• Mshahara PGSS 14
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
- Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
v. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vi. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
vii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
viii. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
ix. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
x. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 24 Machi, 2016
xi. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza..
i. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;
http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’)
ii. MUHIMU: KUMBUKA KUWEKA (TO ATTACH) BARUA YAKO YA MAOMBI KWENYE SEHEMU YA ‘OTHER ATTACHEMENTS’.
iii. VYETI NA WASIFU (CV) VITAKAVYOTUMWA BILA BARUA YA MAOMBI HAVITAFIKIRIWA.
iv. WAOMBAJI WANATAKIWA KUANDIKA MAJINA YA VYUO VYAO NA KOZI KWA KIREFU (Eg. Bachelor of Science with Computer Science, University of Dar es Salaam, na msiandike, BSc. Computer Science UDSM)
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )