Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),imesema haitambui kujitoa kwa Chama cha
Wananchi (CUF),katika uchaguzi wa Mbunge Jimbo la Kijitoupele hapa
Zanzibar unaotarajiwa kufanyika kesho Jumapili licha ya kuwa Tume
imepokea barua rasmi toka kwa uongozi wa Chama hicho.
Mkurugenzi
wa uchaguzi wa Tume ya Taifa Bw Kailima Ramadhani amesema Tume imefikia
maamuzi hayo kutokana na ukweli kuwa barua hiyo ya CUF imechelewa huku
maandalizi ya uchaguzi huo yakiwa yamekamilika na ni Wananchi tu kwa
sasa Wanasubiriwa kwenda kupiga kura.
Aidha
Bw Kailima ameeleza kuwa,kwa kuwa karatasi za kupigia kura
zilishachapishwa na kuwasili hapa nchini tayari kwa uchaguzi
huo,zitaendelea kuwa na picha za Wagombea wa CUF hata kama wamejitoa
katika uchaguzi huo.
Awali,wajumbe
wa Tume ya Taifa ya uchaguzi wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume
Jaji mstaafu Hamid Mahamood Hamid walitembelea katika vituo mbalimbali
vya kupigia kura katika Jimbo la Kijitoupele ili kujiridhisha na
maandalizi ya uchaguzi huo kabla ya uchaguzi kufanyika jumapili.
Tume
ilibaini kuwepo kwa baadhi ya kasoro ndogondogo katika baadhi ya vituo
vya kupigia kura ikiwa ni pamoja na kubanduliwa kwa karatasi zenye
majina ya wapiga kura,mfano katika kituo cha Skuli ya sekondari Kinuni.
Jimbo
la Kijitoupele lina jumla ya Wapiga kura wapatao 17,274 na vituo
vipatavyo 53 vitatumiwa na wapiga kura ili kumchagua mbunge wa Jimbo la
Kijitoupele siku ya Jumapili.
Sambamba
na Uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Kijitoupele, marudio ya uchaguzi
mkuu wa Zanzibar Oktoba 25,2015 ambayo matokeo yake yalifutwa
uatafanyika Jumapili hiyo pia.
Uchaguzi
katika jimbo la Kijitoupele uliahirishwa mwaka jana kutokana na
hitilafu ndogondogo zilizojitokeza katika karatasi za kupigia kura,kabla
ya kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba
25,2015.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )