Pam D
Binti ambaye sasa hakamatiki kwenye
ulimwengu wa muziki Bongo, Pam D amefunguka kuwa, sasa hivi anasitisha
kolabo na wasanii wa kiume akiwemo yule aliyemtoa, Mesen Selekta akidai
kuwa amegundua wanamlemaza.
Akifungukia muziki anaofanya kwa sasa, Pam D alisema, anajua anacho kipaji na anaweza kusimama yeye kama yeye hivyo ni wakati wake sasa wa kutoa ngoma zake kali.
Akifungukia muziki anaofanya kwa sasa, Pam D alisema, anajua anacho kipaji na anaweza kusimama yeye kama yeye hivyo ni wakati wake sasa wa kutoa ngoma zake kali.
“Siwezi kukataa, Mesen kanipa sapoti
kubwa sana mpaka kufikia hapa lakini sasa nimeona nisimame mimi kama
mimi nione nitafika wapi, unajua wakati mwingine ukishirikisha sana
wasanii waliokutangulia, hasa wanaume unajilemaza, kipaji chako
kinashindwa kuonekana vizuri,” alisema Pam D.
Kwa sasa mwanadada huyo anaandaa ngoma
yake mpya baada ya kufanya poa na traki zake zilizotangulia kama vile
Popolipopo na Nimempata.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )