Mahadhi aliyejiunga na Yanga akitokea Coastal Union ya Tanga, alionyesha uwezo mkubwa katika mchezo dhidi ya TP Mazembe, Jumanne ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ambapo alidumu kwa dakika 65 kabla ya kubanwa na misuli iliyosababisha atolewe na nafasi yake kuchukuliwa na Geoffrey Mwashiuya.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mahadhi alisema kwa sasa anajipanga upya kwa ajili ya kuisadia timu yake katika michezo iliyobakia ya michuano hiyo ambayo ni ya pili kwa ukubwa upande wa ngazi ya klabu Afrika hivyo hataki kuipoteza nafasi hiyo.
“Ishu kubwa ilikuwa ni misuli ilinikamata na kusababisha nishindwe kuendela na mchezo japo awali nilikuwa nacheza kwa hofu sana, nikiogopa kuharibu lakini kadiri muda ulivyozidi kwenda nikawa naona kumbe naweza kufanya kitu kwa ajili ya timu yangu ila bahati mbaya ndiyo hivyo sikuweza kuendelea na mchezo ambao kwetu ulikuwa na umuhimu sana.
“Lakini naamini nitakuwa sawa mapema tu Mungu akipenda kwa sababu malengo yangu nimeyaweka katika michezo iliyosalia.
“Kama Mazembe watakuwa kweli wananihitaji basi nitakuwa tayari kwenda kujiunga nao iwapo wataleta ofa ambayo itakuwa na maslahi mazuri maana mimi ni mchezaji na kazi yangi ni mpira sasa fursa ikitokea lazima niitumie,” alisema Mahadhi.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )