Nani mkali zaidi ya Harmonize na Raymond?
Vijana hawa walio chini ya label ya
Diamond, WCB wanafanya vizuri kwa sasa kwa nyimbo zao ‘Bado’ na ‘Kwetu’
lakini kila linapokuja swali la nani mbabe zaidi ya mwenzie, wengi
hupata kigugumizi, akiwemo mshindi wa BSS 2015, Kayumba.
“Mimi wale wote ni kaka zangu, wote napenda kazi wanazofanya,” Kayumba ameiambia Bongo5.
“Mimi sijaona utofauti wowote kati yao,” ameongeza. Kwa upande mwingine Kayumba amesema suala la kufanya nao ngoma haliepukiki.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )