Jumla ya watoto 55 wamefanyiwa upasuaji
katika kambi ya tiba ya watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi,
iliyowekwa katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza siku nne mfululizo,
kufuatia tatizo la kichwa kikubwa walilozaliwa nalo, chini ya udhamini
wa taasisi ya GSM Foundation. Zoezi litakalofanyika katika mikoa mitano
ikiwa ni awamu ya kwanza kati ya nne zinazotarajiwa kufanyika Tanzania
nzima.
Dk Kiloloma
Akiongea wakati wa kufunga kambi hiyo rasmi jioni ya leo, Daktari Bingwa wa upasuaji na mifupa kutoka Taasisi ya Mifupa MOI, Dk Othman Kiloloma, ambaye pia ni mratibu wa kambi hiyo aliishukuru taasisi ya GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni kubwa ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.
Dk Kiloloma
Akiongea wakati wa kufunga kambi hiyo rasmi jioni ya leo, Daktari Bingwa wa upasuaji na mifupa kutoka Taasisi ya Mifupa MOI, Dk Othman Kiloloma, ambaye pia ni mratibu wa kambi hiyo aliishukuru taasisi ya GSM kwa kuamua kulichukua tatizo hilo ambalo ameliita kuwa ni kubwa ukilinganisha na jinsi linavyochukuliwa na jamii ya watanzania.
Dk Kiloloma aliwaambia wanahabari kwamba
jumla ya watoto 2000 huzaliwa na vichwa vikubwa katika kanda ya Ziwa
peke yake, na mtaalamu wa kuhudumia wagonjwa wa namna hii ni mmoja tu
ambapo pia kwa Tanzania nzima, wataalamu wa upasuaji wa watoto wenye
vichwa vikubwa wako tisa tu.
Cha kusikitisha ni kwamba kati ya hao,
ni wachache sana hurudi kwa ajili ya matibabu bali wengi wao hufariki
kwa kufichwa ndani na wazazi wao aidha kwa imani za kishirikina ama
kushindwa kwa wazazi kumudu gharama za matibabu.
Mpaka jioni ya leo, ambayo ni siku ya
nne tangu kuanza kwa kambi hii, jumla ya watoto 55 walikuwa
wameshafanyiwa upasuaji, ambapo siku ya kwanza, walifanyiwa watoto 16,
siku ya pili wakafanyiwa watoto 17, siku ya tatu wakafanyiwa watoto 12,
na leo wamefanyiwa watoto 10.
Mratibu huyo ambaye pia ni Naibu
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI), Dk Othman Kiloloma,
amebainisha kwamba changamoto kubwa inayotokea kwa jamii linapokuja
suala la watoto wenye vichwa vukubwa na mgongo wazi ni gharama za
upasuaji, ambapo gharama ya upasuaji kwa mtoto mmoja ni kati ya shilingi
laki saba za kitanzania mpaka Milioni moja.
“Watoto wengi huzaliwa katika mazingira
duni na wazazi wasiokuwa na nguvu ya kiuchumi, hali inayosababisha wengi
wao kuwaficha ndani huku wakiwahusisha na imani za kishirikina”,
alifafanua Dk Kiloloma.
Dk Kiloloma amesema zaidi ya watoto 4000
huzaliwa kila mwaka wakiwa na tatizo la kichwa kikubwa, lakini
wanaorudi Hospitali kwa ajili ya tiba nhawazidi laki nne, swali kubwa
ambalo jamii hujiuliza ni kuhusiana na watoto ambao hawafiki hospitalini
huishia wapi?
Kwa upande wake, Halfan Kiwamba, Afisa
Mawasiliano wa Taasisi ya GSM Foundation ambao ndio wadhamini wakuu wa
kambi hizo amesema, taasisi yake imeamua kuokoa maisha y watoto hao
ambao ni nguvukazi ya taifa la kesho na inalifanya hilo ikiwa ni moja ya
mikakati yake katika kurudisha fadhila kwa jamii ya kitanzania ambao ni
wateja wakubwa wa bidhaa za GSM.
Kiwamba amesema taasisi yake ina lengo
la kuhakikisha kwamba wananchi wa Tanzania hasa watoto ambao ni wa taifa
ya kesho wanao msingi wa nguvu kazi kwa ajili ya maisha yao ambapo vitu
vikubwa ni elimu boira pamoja na Afya.
Kwa upande wake Meneja wa Taasisi ya GSM
Shannon Kiwamba amesema wakati mwingine ni vigumu kuingia katika maisha
ya kila mwananchi na kumsaidia mahitaji yake, lakini akiwa na uhakika
wa Afya na elimu anaweza kwenda mbali akijumlisha na jitihada zake.
Hivyo amewaomba watanzania kujitokeza wanaposikia taasisi yake inatoa huduma ili kufaidika nayo.
Kambi ya tiba ya GSM inaondoka kesho Mwanza kuelekea Shinyanga ambapo itaweka kambi kwa siku tatu.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )