“Wote nawakubali na tuwaombee wazidi kututangaza zaidi sababu wana 'Fan Base kubwa', aliandika Dogo Janja.
Pia Dogo Janja amesema muziki umemfikisha mbali kutoka kuwa mpiga debe mpaka mpigiwa debe, pale alipoulizwa umefaidika nini tangu alipoanza kufanya muziki.
Mbali na hayo msanii huyo amegusia suala la matumizi ya madawa ya kulevya, alipoulizwa na shabiki wake anachukua hatua gani kupigana na matumizi ya madawa ya kulevya, hususan mtaani kwake alipotokea Ngarenaro Arusha, na kusema kuwa hata yeye anaumizwa na vitendo hivyo, na kutaka wahusika wachukuliwe hatua kwani wanajulikana.
“Mi nahitaji support ya mtaa kuongea na vijana wenzangu, unajua wengi ambao wamejikita humo ni wadogo zangu kaka zangu na baadhi pia ni ndugu zangu inaniuma hata mimi pia, na wanaouza wanajulikana wakamatwe”, alisema Dogo Janja.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )