Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) linapenda kutoa taarifa kwa Umma juu ya uvumi ulioenea katika
mitandao ya kijamii kuwa, limepeleka Wanajeshi wengi visiwani Zanzibar
kwa ajili ya kudhibiti Usalama wakati wa kipindi hiki cha uchaguzi
marudio unaotarajia kufanyika tarehe 20 Machi, 2016.
Habari hizo siyo za kweli na zina lengo
la kupotosha Umma. Kimsingi JWTZ linao Wanajeshi visiwani Zanzibar
wakati wote kwa majukumu yake ya msingi ya Ulinzi wa nchi yetu.
Hivyo hakuna Mwanajeshi yeyote
aliyeongezwa zaidi ya wale waliopo visiwani humo tangu awali. Taarifa
hizo zipuuzwe,zisipewe nafasi yoyote ya kujenga hofu kwa Wananchi.
JWTZ linapenda kwa mara nyingine tena
kuwahakikishia Wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi wowote kuhusu ulinzi na
usalama wa nchi yetu, kwani wakati wote Jeshi lao lipo imara kuwalinda.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638.
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )