Ripoti ya World Economic Outlook ‘WEO’ ambayo inatoa makadirio ya maendeleo ya kiuchumi
katika ngazi ya kimataifa, ripoti hiyo hutolewa April na
September/October kila mwaka ambapo hutumia database kupata taarifa za
akaunti za taifa, mfumuko wa bei, viwango vya ukosefu wa ajira, bei za
bidhaa n.k.
Katika
ripoti yake ya April 2016 imeitaja nchi ya Myanmar kuwa ndio nchi
inayoongoza kwa ukuaji wa kiuchumi kwa haraka zaidi kwa pato
linalokadiriwa kukua kwa 8.6% kwa mwaka.
Ivory
Coast imekuwa nchi ya pili na makadirio ya ukuaji wa pato la Taifa la
8.5% mwaka huu. Nchi zingine zilizotabiriwa kurudi takwimu ya juu ya
ukuaji ni pamoja na India, Laos na Tanzania.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )