Kampuni ya Mohammed Enterprises
Tanzania Limited (MeTL) imekanusha taarifa ambayo ilitolewa na baadhi ya
vyombo vya habari kuwa kampuni hiyo imeficha sukari tani 2,990 katika
Bandari Kavu (ICD) ya PMM iliyopo Vingunguti, Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imekuja baada ya Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutembelea ICD na kukuta tani
2,990 ambazo aliambiwa kuwa ni mali ya Mohammed Enterprises jambo ambalo
halikuwa na usahihi bali ni mali ya Tanzania Commodities Trading
inayomilikiwa na Murtaza Dewji.
Kwaa mujibu wa Murtaza Dewji ambaye
ndiyo mmiliki wa sukari hiyo amesema kuwa sukari hiyo iliingia nchini
kwa kufata utaratibu wote kama jinsi inavyotakiwa na anashangazwa
kwanini hakufatwa ili kutoa maelezo kuhusu sukari hiyo.
“Tulifuata taratibu zote zikiwepo
mamlaka husika za nchi kma bodi ya sukari, Mamlaka ya Chakula na Dawa
(TFDA) na vyombo vyote vya ulinzi na usalama,” amesema Murtaza.
Akifafanua zaidi amesema kuwa sukari
hiyo ilikuwa njiani kuelekea nchini Uganda na vielelezo vyote vipo
lakini kutokana na uhaba wa sukari nchini, serikali iliagiza mzigo huo
kubaki nchini na kuingiza sokoni ili kumaliza tatizo hilo ambapo
ulitakiwa kuanza kuingia sokoni kati ya Mei, 12 na Mei, 13.
Aidha ameelezea kuwa ni jambo la
kawaida kuagiza sukari kutoka Dubai kwani hutumia siku 7 pekee kufika
nchini tofauti na sukari kutoka Brazil ambayo hutumia siku 50 hadi 60
ikiwa njiani hadi kufika nchini.
“Wafanyabiashara wote wanaojua
biashara walioko karibu na Dubai hufanya hivyo na sisi sio wa kwanza
kuagiza sukari kutoka kwa wauzaji wa Dubai,” amesema Murtaza.
Pia Murtaza amewatoa hofu Watanzania
kuhusu uhaba wa sukari kwa kusema kuwa tayari sukari imeagizwa na ndani
ya wiki mbili kutakuwa na sukari ya uhakika nchini hivyo kuwataka
kuondoa hofu iliyokuwapo hapo awali.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )